BAADHI ya wasanii wa filamu za Kibongo hivi karibuni walinaswa
wakifanya vitendo vichafu katika eneo lao la kurekodia ‘location’ pande
za Oysterbay jijini Dar, Ijumaa lina uthibitisho wa kutosha.
Kwa mujibu wa chanzo chetu wasanii hao walinaswa wakifanya vitendo
hivyo vilivyo nje ya maadili ya Mtanzania kwa uwazi bila ya kumuogopa
mtu yeyote.
Chanzo chetu kilijipenyeza katika kambi ya wasanii hao iliyopo eneo hilo na kuwanasa wakifanya vitendo hivyo vichafu.
Chanzo chetu kilijipenyeza katika kambi ya wasanii hao iliyopo eneo hilo na kuwanasa wakifanya vitendo hivyo vichafu.
“Wameweka kambi kwenye nyumba moja Mikocheni na wamekuwa wakienda
kushuti kwenye Ufukwe wa Coco, yaani nimekuwa nikiwafuatilia matendo
yao, siyo mazuri. Wanavaa nguo nusu utupu, wanafanya vitendo
vinavyoashiria usagaji mbele za watu bila aibu, njooni muwafichue.
“Kuna picha ambazo nimewapiga bila wao kujijua, zinatia kinyaa, mbaya
zaidi wengi wao ni wadogowadogo na huenda wamewadanganya wazazi wao
kuwa wameenda shule kumbe wapo huku,” kilisema chanzo hicho.
Sign up here with your email