Huyu ndie mfungwa aliefariki dakika 13 baada ya kuchomwa sindano, kisa mauaji ya huyu binti

 Mfungwa mmoja amefariki Marekani kwa mshtuko wa moyo baada ya kuchomwa sindano yenye lethal (lethal injection) yenye Mchanganyiko wa dawa tofauti kwa ajili ya kuua. Clayton Lockett alitakiwa kuuliwa baada ya kesi ya mauaji katika gereza la Oklahoma lakini kabla ya hapo alichomwa sindano hiyo na kufariki baada ya dakika 13.
Wiki iliyopita Lockett na mfungwa mwingine walipangiwa kuuliwa kupitia dawa hiyo ya lethal ambapo mahakama ilithibitisha dawa hiyo inakidhi mahitaji ya katiba lakini baada ya madhara kutokea kwa Lockett, mfungwa mwenzake walietakiwa kuuliwa pamoja ameongezewa siku 14 mbele.
Screen Shot 2014-05-01 at 9.29.35 PMBaada ya Lockett kufariki Wamarekani wengi wametoa maoni yao na kusema hukumu hiyo ya kifo kwa Lockett ni sawa kabisa kutokana na makosa aliyoyafanya.
Lockett alifungwa baada ya kuua msichana mwenye umri wa miaka 19 aitwae Stephanie Neiman kwa kutumia bunduki aina ya shotgun kutokana na msichana huyo na rafiki yake kumsumbua wakati akiiba katika nyumba ya mtu vilevile mahakama iligundua Lockett alimzika msichana huyo na kisha kumbaka rafiki yake aliebaki.
Baada ya kuchomwa sindano Mwili wa Lockett ulikuwa ukitetemeka kwa muda wa si chini ya dakika 13 kabla ya kufa kwake ambapo kifo chake kimetafsiriwa kama kifo cha uzembe ambapo kumefanya kusimamishwa kwa mauji ya aina hiyo baada ya kuonekana sindao hiyo haifanyi kazi inavyotakiwa.
Marehemu Stephanie Neiman wiki mbili kabla ya kifo chake.
Marehemu Stephanie Neiman wiki mbili kabla ya kifo chake.
Wasimamizi wa mauaji hayo walianza kufunga mapazia ya chumba hicho baada ya kuona Lockett akizidi kuwewesuka ambapo mmoja wa mashahidi wa kitendo hicho amesema aliweza kuhisi jinsi Lockett alivyokuwa akiumia na haikua njia ya kawaida kwa kuua mtu hata kama ana kosa gani.
Dawa hizo zilimfanya Lockett aonekane akizungumza bila ya kukamilisha hata neno moja.

Previous
Next Post »

Blogger templates