KAJALA "NAIGOPA SIMU YANGU" ADAI UGOMVI WAKE NA WEMA UMEKUZWA NA WATU



Muigizaji wa filamu nchini, Kajala Masanja amesema kutokana na jinsi ambavyo ugomvi wake na Wema Sepetu ulivyokuwa mkubwa, amefikia hatua anaigopa simu yake zaidi ya kupiga na kupokea.

Akiongea kwenye kipindi cha Take One cha Clouds TV wiki hii, Kajala amesema amekuwa akiumizwa na jinsi anavyotukanwa kwenye mitandao ya kijamii kutokana na ugomvi huo. Kajala amesema ugomvi wake na Wema haujatokana na kile kinachodaiwa kuwa alimchukulia ‘bwana yake’ na kwamba umetokana na vitu vidogo ambavyo ni binafsi kwao. Amesema pamoja na ugomvi wao kusababisha na mambo ya kawaida, umekuzwa mno na watu pamoja na vyombo vya habari kiasi cha kuwafanya wajikute maaudui kweli.

Kuhusiana na tetesi kuwa alianza kumdharau Wema baada ya Miss Tanzania huyo wa zamani kuishiwa fedha, Kajala amesema amekuwa rafiki yake tangia enzi hana chochote. “Alikuwa rafiki yangu kabla hana kitu, kwahiyo kwamba nilianzisha urafiki na Wema kwasababu alikuwa na hela lakini sasa hivi hana hela mimi sio rafiki yangu tena, sio kweli,” amesema.

Kajala amekiri kuwa kukosana kwake na Wema kumeathiri maisha yake.

“Inaniathiri sana kwasababu ni mtu ambaye nimemzoea, mtu ambaye tumefanya vitu vingi kwahiyo sometimes nikikaa nammiss,” amesema.

Kajala ameeleza kuwa ameshawahi kumtaka Wema wamalize ugomvi wao lakini ilishindikana japo amesema kwakuwa ugomvi ni wao wenyewe, ipo siku utaisha na watakuwa marafiki tena.
Previous
Next Post »

Blogger templates