KUVUJISHA NYIMBO NDIO SABABU YA MANECKY KUMTOSA DIAMOND


INASEMEKANA ile tabia ya kuvujisha nyimbo inayofanywa na msanii wa muziki wa kizazi kipya Diamond Platnum imeonekana kuwa ndiyo sababu ya mtayarishaji wa muziki huyo Manecky kuacha kufanya kazi pamoja na msanii huyo.

Manecky aliamua kufikia maamuzi hayo ya kusimama kufanya kazi pamoja na msanii huyo kwa madai kuwa kuvujisha kwa nyimbo ambazo bado hazijakamilika kungeweza kumuaribia kazi.

Akizungumza katika mahojiano na Global TV mtayarishaji huyo aliweka wazi kuwa baadhi ya wasanii akiwemo na Diamond wamekuwa na tabia ya kuvujisha nyimbo zao wenye ambazo bado hazijamalizika kutengenezwa.

“Baadhi ya wasanii wanatabia ya kuomba kazi ambazo hazijamalizika na kuiweka kwenye simu yake na kuanza kusikilizisha marafiki zao na ndio kilichotokea kwa Diamond” alisema Manecky.

Aliweka wazi kuwa tabia hiyo ndiyo iliyopelekea yeye kuacha kufanya kazi na msanii huyo kwa kuogopa kuharibu kazi zake kwani yeye yupo katika biashara


ambayo anategemea kupata faida!!
Previous
Next Post »

Blogger templates