WANAMGAMBO wa
Al Shabaab wamedai kuwa wamemuua kwa kumfyatulia risasi mbunge maarufu
mjini Mogadishu. Taarifa zinasema, Ahmed Mohamud Hayd (Mb) aliuawa baada
ya kutoka hotelini ambapo katika tukio hilo, mlinzi wake pia aliuawa
huku Katibu wa Bunge akibaki amejeruhiwa.
Kundi la Al-Shabaab, ambalo lina
uhusiano na lile la al-Qaeda, limeapa kuendelea na mashambulizi zaidi
katika kipindi hiki cha mwezi mtukufu wa Ramadhani. Wanamgambo hao
walipoteza ngome yao mjini Mogadishu na kuchukuliwa na Vikosi vya Umoja
wa Afrika mwaka 2011, lakini wameendelea na mashambulizi ya mabomu na
mauaji mjini humo.
Msemaji wa kundi hilo, Abdulaziz Abu
Musab alisema kuwa kundi lake limemuua kama ilivyopangwa na kuwa
wataendelea kuwafuatilia wabunge wengine ikiwa hawataachana na Bunge
nchini humo. Al-Shabaab imekua ikipigania kuunda taifa la kiislamu
nchini Somalia.
Sign up here with your email