Picha
zinazoonyesha jinsi mtangazaji wa kituo cha Redio cha Times, Khadija
Shaibu alivyochezea kichapo kutoka kwa mumewe, Edzen Jumanne zimevuja.
Majeraha katika mwili wa Dida baada ya kipigo kutoka kwa mumewe Ezden.
Picha hizo zinamuonesha Dida akiwa na majeraha makubwa sehemu mbalimbali za mwili wake ikiwemo mkononi, kichwani na mapajani.
Dida.
Akizungumzia
kipigo hicho hivi karibuni, Dida alidai kuwa, baada ya kutofautiana
kufuatia wivu wa kimapenzi, mume wake huyo baada ya kumporomoshea
mitusi, alichukua mkanda wa suruali na kumpiga nao hadi kumsababishia
majeraha hayo hali inayomfanya muda mwingi avae kininja kuficha aibu.
Mpaka sasa wawili hao kila mmoja kivyake huku ndoa ikielezwa kuwa haipo tena.
Sign up here with your email