Tafadhali weka mawazo yako hapa ili uweze kumgundua mwenzi ambaye ni mwizi wa haki yako. Sasa hebu twende tukaone.
RATIBA YA GHAFLA
Rafiki
zangu, ukishaanza kuwa na wasiwasi na mpenzi wako kwamba huenda anataka
kukusaliti, jambo la kwanza kabisa unalotakiwa kukumbuka ni sehemu
aliyokuambia amepitia/anakwenda kama ilikuwa katika mipango yake au
amefanya safari ya kushtukiza.
Hii ni
dalili ya kwanza kabla hata hamjakutana nyumbani; “Sorry baby, kuna
sehemu napitia mara moja, nitachelewa kidogo kurudi nyumbani,” kauli
kama hii iangalie sana.
Mwingine
anaweza kupiga simu na kusema: “Mume wangu, bosi ametupa ofa ya dina
wafanyakazi wote, kwa hiyo nitachelewa kurudi nyumbani, samahani sana
dear.”
Kauli
hizo mbili ni alama ya kwanza katika kushibisha hoja yako ya kusalitiwa
kama ni kweli atakuwa amefanya hivyo. Kumbuka kwamba, si lazima kila
anayesema amepata dharura amesaliti.
ANAKWEPA KUWASILIANA
Mtu
huyo ambaye ameshatoa taarifa kwamba amepata dharura, utashangaa hataki
kuwasiliana na wewe. Pengine ukimpigia simu, anaweza asipokee na kama
akipokea anaweza kukujibu: “Nitakupigia baadaye, samahani sipo sehemu
nzuri.”
Unaweza
kumwandikia meseji lakini pia asijibu. Wapo wengine vichwa ngumu zaidi,
ambao wao kuacha kupokea simu na kujibu meseji si vitu muhimu sana,
wanazima kabisa! Ukiona dalili hii, basi ujue unasalitiwa.
UCHANGAMFU KUPITILIZA
Pamoja
na mambo hayo hapo juu, lakini mwenzi huyu akirejea nyumbani, huwa
mchangamfu kupitiliza. Ana maneno mengi, anaanzisha mijadala ya ghafla
na kuifunga mwenyewe. Atajifanya anataka kufanya mambo mengi kwa ajili
yako.
Ahadi
zake zinakuwa nyingi za ghafla na nyingi zipo wazi kabisa kwamba si
rahisi kuzitekeleza. Alama hii ni kati ya zile 10 zinathibitisha kwamba
ndani ya saa 24 umeibiwa mali yako.
UPOLE KUPITILIZA
Kinyume
cha uchangamfu ni upole, kama mwenzi wako ametoka kimapenzi na patina
mwingine kwa ile hofu yake moyoni, anaweza kuwa mpole kupitiliza.
Anafanya hivyo kwa lengo la kutafuta huruma.
Hana
sababu ya kuwa mpole, lakini anaweza kutumia ngao hiyo, ili maswali
utakayomuuliza yawe kuhusu upole na ukimya wake, usahau mambo ya kuhisi
kuwa umesalitiwa. Hata hivyo, majibu yake yanaweza kuwa ya mkato sana:
“Sijisikii vizuri, siku yangu haikuwa nzuri kabisa leo. Kuna mtu
nimetibuana naye ofisini, amenichanganya kabisa.”
Alama hii
ni moja ya sababu zitakazokufanya uendelee kumchunguza katika hatua
zinazofuata ili mwisho ugundue kuwa umesalitiwa au ni wasiwasi wako tu.
UGONJWA WA GHAFLA
Katika
kukwepa usumbufu wa maswali mengi, mwingine huamua kujifanya anaumwa.
Atarudi akiwa mkimya kuliko kawaida, ukimwuliza atakujibu kuwa anaumwa.
Kama mpenzi wake, anajua wazi kuwa hutakuwa na muda wa kuanza kuhisi
usaliti badala yake utamjali na kuuliza hali yake.
Mgonjwa
huyu kwa kawaida huwa haumwi magonjwa siriasi, sana sana atakuambia
hajisikii vizuri, kichwa kinamgonga au moyo unaenda mbio. Ukizungumza
kuhusu suala la hospitali atakataa akidai hana hali mbaya sana. Mara
nyingi hupenda kukimbilia kitandani, akitaka kupumzika.
Anafanya
hivyo kwa sababu anakwepa aibu ya kukutanisha uso wake na wako. Ukitaka
kwenda kumnunulia dawa za maumivu atakujibu: “Nimeshameza panadol baby.”
Mwenzi wa aina hii unatakiwa umtilie mashaka, maana inawezekana ametoka
kufanya kitu kibaya.
MAJIBU TATA
Mpenzi
ambaye ametoka kukusaliti huwa hapendi kuulizwa maswali mengi,
ukimwuliza majibu yake huwa tatanishi sana. Kwa kuwa ameshasingizia
kwamba anaumwa, hivyo atafika na kulala moja kwa moja.
Ukitaka
kujua zaidi kuhusu kuugua kwake au dharura aliyoipata iliyosababisha
achelewe kurudi nyumbani, hukosa majibu yanayoeleweka. Wakati mwingine
anaweza kujisahau na kukupa jibu ambalo linapingana na maelezo yake ya
awali. Ukiona hivyo ujue kuna namna.
HATAKI FARAGHA
Kwa
kuwa tayari ameshatoka kwa mtu mwingine, huhofia sana kukutana na wewe
faragha. Kama tulivyoona katika vipengele vilivyopita, hutengeneza
mazingira ya kukufanya msikutane kimwili, hofu yake ikiwa ni kukuficha
usigundue mchezo wake mchafu.
Kisingizio
cha kuumwa, bila shaka ni kikubwa na kitakufanya ushindwe kuwa na
mhemko wa kimahaba, lakini kurudi nyumbani akiwa amekunja ndita au mpole
kupitiliza, tafsiri yake ni wewe kuogopa au kuhamisha hisia zako kutoka
kwenye mapenzi na kuanza kumfikiria yeye kama yeye.
Kwa
vyovyote vile, kama ni mwenzi wako wa muda mrefu, zipo alama nyingi
zitakazoweza kukufanya ujue kuwa ametoka nje, kwanza ni vyema kumkazania
kukutana naye faragha. Hata kama atasingizia anaumwa, ng’ang’ania
kukutana naye, maana hapa ndipo penye ukweli mkubwa zaidi.
Mchunguze
anavyokupokea, halafu pima uwajibikaji wake. Huwa mvivu na asiyetaka
kutoa ushirikiano. Anaweza kuishia kulalamika kuwa hajisikii vizuri na
kusisitiza mhairishe zoezi hilo.
Mpenzi
msomaji, njia unayopita kila siku unaijua. Sehemu yenye makorongo
unaifahamu, yenye matuta pia utatambua, hata yenye makorongo yenye maji
yaliyosimama pia unaijua vyema, sasa ukikutana na tofauti yoyote katika
barabara unayoitumia siku zote, maana yake tingatinga limepita.
ANAKWEPA KUSOGELEWA
Akifika tu nyumbani, atahakikisha hupati nafasi ya kuwa naye karibu. Hataki kabisa kusogelewa. Hapo anakimbia vitu vitatu;
Kwanza kabisa, inawezekana huko alipotoka alitumia manukato tofauti na aliyotoka nayo nyumbani asubuhi.
Pili,
manukato ya sabuni mpya aliyotumia, anaogopa usiyasikie, tatu, kila mtu
ana harufu yake, unapokaa na mtu kwa ukaribu hasa faragha kwa saa mbili
au zaidi, kila mmoja huhama na harufu ya mwenzake.
Kwa kuwa
wewe unaitambua vyema harufu ya mpenzi wako, atahofia kukusogelea maana
utashtukia. Mwisho kabisa, hata kama atakuwa amekwepa yote hayo, labda
hajaoga, hajatumia manukato mengine, bado utaweza kumkamata kwa harufu
ya manukato, sabuni au mafuta aliyotumia mtu aliyekuwa naye.
Kukwepa
kukusogelea, tafsiri yake ni kwamba hataki usikie harufu ya tofauti
kutoka kwake, maana anajua alichokifanya. Jiulize, kama kila siku huwa
mnapokeana kwa mabusu na kukumbatiana, kwanini safari hii anakukwepa?
ANAKIMBILIA BAFUNI
Akifanikiwa
kukuzuga katika kipengele kilichopita, basi safari yake huishia bafuni.
Ataenda haraka na hatataka kwenda na wewe maana kuna kitu anajaribu
kukuficha. Wengi wanaamini (kuna ukweli kwa asilimia chache) baada ya
kuoga wanaweza kupoteza ushahidi wa kutoka nje ya ndoa/wapenzi wao.
Utakapomruhusu
aoge, kwanza atatumia sabuni ya siku zote, ambayo anaweza kuitumia kwa
wingi awezavyo ili kuficha ushahidi. Atajisafisha zaidi nyeti zake ili
usijue kilichotokea muda mfupi.
Akitoka
bafuni lazima atakimbilia kwenye meza ya kujipambia kisha hapo
atajimiminia manukato ili kuzima kabisa ushahidi ambao ungeweza
kumuumbua. Jiulize, kama kila siku huwa mnaoga pamoja, kwanini amekuja
ghafla na kukimbilia bafuni bila wewe?
WASIWASI MWINGI
Atakuwa
mwenye wasiwasi mwingi sana, hata kama akikubali kukutana na wewe
faragha, ushirikiano huwa hafifu. Mwoga kupitiliza na muda wote huwa
anahisi kwamba hatakufikisha salama safari yako.
Wasiwasi
wake hauishii hapo, hata kupeana mikono tu na kukutanisha macho,
kutakuonesha jinsi alivyo na wasiwasi. Si kama anapenda hali hiyo, ila
anazidiwa na hisia za usaliti kwa kuwa anajua alichokifanya muda mfupi
uliopita.
Kama
utavifuatilia vipengele hivyo kwa makini, ni rahisi sana kumkamata mwizi
wako. Acha papara, chunguza taratibu, ukiona angalau kuna nusu ya hizi
nili zokupa hapo juu, ujue wazi kuwa unaibiwa tu
Sign up here with your email