Muigizaji mwanamke nchini Marekani aliyemtumia Rais Barack Obama barua iliyokuwa na sumu ya Ricin amefungwa jela kwa miaka 18.
Shannon Richardson, mwenye umri wa miaka 36, kutoka Texas, pia alimtumia meya wa New York Michael Bloomburg barua nyingine iliyokuwa na sumu hiyo hiyo.
Alidai kuwa mumewe waliyeachana naye ndiye alituma barua hizo katika njama ya kumlimbikizia madai hayo.
Shannon aliambia mahakama.
Alikiri kosa la kumiliki na kutengeza sumu hiyo mwezi Disemba.
Jaji alimpa hukumu kubwa zaidi ikilinganishwa na kosa lake na pia kutakiwa kulipa faini ya dola 367,000.
Richardson, mama mwenye watoto six, ameigiza katika vipindi kama 'The Vampire Diaries' na 'The Walking Dead.'
Viongozi wa mashitaka wanasema kuwa mwanamke huyo aliagiza bidhaa za kutengeza sumu hiyo kupitia kwa mtandao kisha akatuma barua tatu zilizokuwa zimepakwa sumu hiyo.
Kulingana na viongozi wa mashitaka, moja ya barua alizomtumia Obama , ilikuwa na maandihsi haya:
Barua nyingine iliyopokewa na meya Bloomberg, anayeunga mkono kudhibitiwa kwa bunduki, ilisema,
Barua ya tatu iliyokuwa na kemikali hiyo ya sumu, ilifunguliwa na bwana Mark Glaze, mkurugenzi mkuu wa idara inayofadhiliwa na Meya ya kupambana na silaha haramu.
Richardson katika kumtaka jaji kumhurumia, aliomba msamaha akisema,
Aliomba msamaha na huruma na kusema tayari anahisi ameadhibiwa vya kutosha kwa kunyang'anywa watoto wake sita
Sign up here with your email