NAOMBENI USHAURI WENU,PAMOJA NA UTUNDU WANGU WOTE WA MAPENZI NIMEPIGWA KIBUT

Naitwa hilda nina miaka 24 nilijiingiza kwenye mahusiano namvulana mmoja ambaye nampenda sana tulikua tunasoma wote chuo kimoja baada ya kumaliza chuo kila mmoja akaenda kwao tuliagana vizuri, akaniahidi kuwa baba wa wanangu baada ya muda. Kila mmoja akiwa kwao mawasiliano yakawa yamepungua nikawa namlalamikia sana juu ya yeye kutokunitafuta. 
Rafiki nisikufiche huyu mvulana nampenda sana hili lilinipelekea kuwa na wivu sana juu yake nikahisi naibiwa kwa sababu tulipokua wote chuo alipenda kuniambia ananipend sana ila baada ya kuagana hakuwa ananiambia tena. Siku moja nikamuuliza kwa nini hanitamkii tena kama ananipenda hakunipa jibu la moja kwa moja nakumbuka hiyo siku nilimlalamikia sana. 
Siku moja akanitumia sms akaniambia amechoka kulaumiwa hataki tena uhusiano nililia nikajaribu kumplease akakataa akasema anataka tuwe marafiki tu. Kiukweli nampenda sana natamani arudishe moyo wake kwani ni yeye wa pekee katika moyo wangu.
Previous
Next Post »

Blogger templates