BOFYA HAPA UONE ISHARA 7 ZA KUACHWA NA MPENZI WAKO


Mwanamke ni kiumbe wa ajabu sana. Huwa anahitaji amani ya moyo, furaha na kusikilizwa sana. Ikitokea anavikosa hivyo anavyovihitaji huongea maneno flani ambayo na machache sana na yanaonekana madogo mno, ila kiukweli yana maana kubwa sana katika mahusiano yenu. Ukiyapuuzia maneno na misemo hiyo, muda si mrefu, utasalitiwa ama kuachwa!!
Yafuatayo ni maneno na misemo ya wanawake inayoh

ashiria kuvunjika ama kuathika kwa mahusiano ya kimapenzi:

1. Mwanamke anaposema, 'sasa hivi' au'dakika moja tu,' lakini ikawa ni nusu saa ijayo, jua kuna tatizo kwenye mahusiano yenu. Ukiona hilo linaongeka na kudumu kiasi cha wewe kutokumwamini, alafu pia hakuambii samahani kwa kutokujali promise, jua kuna tatizo kubwa kwa sasa.

2. Mwanamke anaposema, 'utajua mwenyewe,' ana maana kwamba amekasirishwa na kukatishwa tamaa na tabia yako na sasa hajali tena. maana yake ni kwamba kwa upande wake haoni sababu ya kujiumiza bure na huenda atachukua uamuzi ambao nawe pia hautaufurahia. Je, anaweza kuanza kutoka nje baada ya hapo? inawezekana ingawa siyo lazima.

3. Mwanamke anapopumua kwa nguvu, yaani kushusha pumzi kwa kishindo,“huuuuuuuuuuuu” hiyo pia ni kauli kwa upande wake. kama anashusha pumzi kwa nguvu wakati mkijadili au kuongea jambo, ni taarifa kwamba amekudharau. yaani amekuona mjinga nambari moja. ni kauli kwamba, haoni sababu ya kuendelea kuwepo hapo kubishana nawe, kwani huna jambo la maana lamweleza.

4. Mwanamke anapotumia neno,'sawasawa,' kwa kawaida kama kuna jambo umemfanyia, ina maana kwamba, 'ninachukua muda kutafakari, halafu utaona nitakachokulipa baadaye.' Kauli hii siyo nzuri na mara nyingi ni ya hatari. Wanaume ambao wamewahi kulipiziwa visasi kwa njia mbaya na ya hatari na wapenzi wao wamekiri kuambiwa,'sawasawa,' au 'sawa bwana,' kabla ya visasi hivyo.

5. Mwanamke anapotamka neno, 'we endelea tu,' anakuwa na maana ya kwamba, siku si nyingi zijazo atafanya jambo ambalo hutalifurahia, kama hutaacha kufanya kitu au jambo lenye kumuudhi. Hiyo ni kauli ya kukutahadharisha kwamba, usije ukashangaa pale ambapo utaona amefanya kitendo cha hatari dhidi yako kutokana na tabia yako au matendo yako mabaya dhidi yake.

Most popular tags for this image include: skinny, beautiful, black girl, dimples and girl




6. Kuna wakati mwanamke anaweza kusema,'sawa bwana, fanya,' kama kuna jambo ambalo hamjafikia muafaka au amebaini umekuwa ukifanya jambo fulani baya au lenye kumkera. Hapa hana maana kwamba, amekuruhusu kwa moyo mmoja, hapana. Hapa anataka ubaini kwamba, hajakubaliana nawe, anakupa muda wa kujaribu kutafakari tena.

7. Je, kama mmeshindana katika jambo au umemkera katika jambo au mambo fulani, kutokana na tabia au mwenendo fulani, halafu akikuambia, 'asante sana,'? Itakuwa na maana gani? Hii ina maana umemkera kupita kiasi na bado wala hajajua akufanye nini. Hii ni toafauti na 'asante' ya kawaida. Mwanamke anapoongeza neno 'sana,'ujue umemkera hasa, kuliko unavyoweza kufikiri. Halafu kama baada ya kusema, 'asante sana,' anashusha pumzi kwa nguvu, ujue hali ni mbaya zaidi, bora unyamaze kwanza, hata radhi usiombe kwa muda huo, subiri apoe kwanza
Previous
Next Post »

Blogger templates