Watu 93 wakamatwa kwa kuvamia shule Jijini Mbeya

Jeshi la polisi Jijini Mbeya linawashikilia wananchi wa kijiji cha Lupembe Wilayani Kyela wapatao 93 kwa kuvamia shule ya sekondari Mwingo wakiwa na silaha mbalimbali za jadi.
 
Wananchi hao wamefanya uvamizi huo kwa kile kinachoelezwa kuwa walikuwa wakiwataka walimu na wanafunzi wa shule hiyo waondoke katika eneo la shule wanalodai kuwa ni mali ya kijiji.
Kwa mujibu wa kaimu kamanda wa polisi mkoa wa mbeya Kamishana msaidizi wa polisi Barakael Masaki amesema Chanzo cha fujo hizo ni Mgogoro wa mpaka wa shule hiyo na eneo la kijiji.
polisiKamishana Masaki ametoa wito kwa jamii kufuata sheria katika kudai haki zao kwa njia ya amani na utulivu ili kuepukana na matatizo yanayoweza kuepukika.
Previous
Next Post »

Blogger templates