MSANII DIAMOND AHOJIWA POLISI, ASALIMISHA MAGWANDA YA JESHI, AACHIWA KWA DHAMANA

MSANII wa Muziki wa Kizazi kipya nchini,Naseeb Abdul  maarufu kama Diamond Platnumz amehojiwa na Jeshi la Polisi baada ya kuonekana na mavazi halisi ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) katika Tamasha la Fiesta lililofanyika jijini Dar mwishoni mwa wiki.
Diamond amejikuta hapo  siku moja tu baada ya Meneja wake Babu Tale kukamatwa  jana kwa kuhojiwa na kulala mahabusu kuhusiana na matumizi hayo ya mavazi ya kijeshi katika onyesho la Fiesta.
Habari zinasema Diamond naye alijisalimisha mwenyewe polisi ambako baada ya mahojiano aliachiwa kwa dhamana. Magwanda aliyokuwa nayo aliyakabidi polisi wakati uchunguzi ukiendelea
Previous
Next Post »

Blogger templates