MAMLAKA
ya Udhibiti wa Mawasiliano hapa Nchini (TCRA) imewaonya watumiaji wa
mitandao ya kijamii wanaojisajili katika mitandao hiyo kwa kutumia
majina na taarifa za uongo.
James
Kilaba Kaimu Mkurugenzi wa TCRA amesema, vitendo vya watu kujisajili
katika mitandao ya kijamii kwa kutumia majina na taarifa zisizo sahihi,
ni kosa kisheria na kwamba wanaofanya hivyo watachukuliwa hatua kali za
kisheria.
Kilaba
ameyasema hayo jana, wakati wa uzinduzi wa kampeni ya kuongeza ufahamu
kuhusu matumizi sahihi na salama ya mitandao ambayo inasimamiwa na
Kitengo cha dharura cha kuitikia matukio ya usalama kwenye mitandao hapa
nchini (TZ-CERT).
“Tumeamua
kuzindua kampeni hii ili kuwasaidia wananchi kuepuka makosa ya
kimtandao na kuepuka kufanyiwa utapeli au wizi mitandaoni kwa sababu
matukio mengi ambayo yamekuwa yakiripotiwa au kulalamikiwa yanazuilika
kwa watu kupewa elimu ya matumizi sahihi ya mitandao,” alisema Kilaba.
Kampeni
hiyo ya kuongeza ufahamu kuhusu matumizi sahihi na salama ya mitandao,
itafanyika kupitia matangazo ya redio, televisheni, magazeti pamoja na
mitandao ya kijamii ambapo katika mitandao ya kijamii itajulikana kama,
“Darasa mtandao”.
“Miongoni
mwa mambo ambayo tutawafundisha wananchi ni kutoweka wazi taarifa zao
binafsi zote katika mitandao, kubadili na kutunza neon la siri
(password), kutojibu ujumbe unaosema umeshinda bahati nasibu na
mengineyo mengi,” alisisitiza Kilaba.
Sign up here with your email