Mayweather avunja pigano na mpiganaji Conor Mc Gregor

Bondia Floyd Mayweather ambaye amestaafu, amesema kuwa pigano kati yake na mpiganaji Conor Mc Gregor halitofanyika.
33f3b9f400000578-3584787-image-a-14_1462971677202
Bingwa huyo wa mizani mitano tofauti wazamani, mwenye umri wa miaka 39 alisema mapema mwaka huu kwamba angependa kupigana na nyota huyo wa Ireland.
”Nilijaribu kuona pigano hilo linafanyika,lakini hatukuweza kwa hivyo tunasonga mbele”.Mayweather aliambia FightHype.com.
”Nafurahia kuwa na heshima kubwa katika masumbwi na wala sipigani tena”.
McGregor awali alikuwa amesema kuwa alivutiwa na pigano hilo ,lakini ilitarajiwa kuwa Mayweather angetafuta kiasi cha fedha anazotaka ili pigano hilo lifanyike
Previous
Next Post »

Blogger templates