Wanafunzi UDSM Waitupia Lawama Bodi ya Mikopo

Mwisho mwa wiki iliyopita wizara ya elimu ilitangaza majina ya wanafunzi watakaopata mikopo na vigezo vilivyotumika ikiwemo wanafunzi waliosoma masomo ya sayansi, walemavu, yatima, pamoja na ufaulu wa waombaji huku vigezo hivyo vikiwaacha nje wanafunzi wanaochukua masomo ya sanaa.

Wakizungumzia mabadiliko hayo, wanafunzi wa chuo kikuu cha Dar es Salaam, UDSM, wamesema hakuna aliyetarajia kutokea kwa hali hiyo kwani hawakutangaziwa mapema kwamba utaratibu wa utoaji mikopo umebadilika. Wengine wamedai kuwa wazazi walikuwa wamekwisha wasafirisha watoto kutoka mikoani wakitegemea udhamini kutoka bodi hiyo.

Naibu waziri wa mikopo UDSM, Abdul Nondo amesema, “Ukiangalia taarifa ambayo imetoka bodi ya mikopo kwamba itatoa fedha kwa wanafunzi ambao watasoma Sayansi,itatoa fedha kwa yatima,itatoa fedha kwa walemavu wale ambao ni maskini. Wamesema shule za kata kwa kulipa ada shilingi elfu 20/70 mpaka kufika chuo sasa hivi na kufanya vizuri. Wanapewa vigezo vya kutopewa mikopo na kubaguliwa kwamba as if they are not students.”

Kwa upande wake waziri wa mikopo wa UDSM, Kasunzi Eliud alisema, “Unaweza ukafika kuna mwanafunzi wa sayansi ni daktari lakini ametokea katika familia tajiri, tunasema familia inayojiweza. Lakini mimi mtoto wa mkulima ambaye nimeweza kusoma kwa shida kwa kuungaunga pesa mpaka nikafika chuo kikuu, leo hii vigezo vinakuja kutoka kwamba mwanafunzi anayesomea masomo ya arts hawezi kupata mkopo.”
Latest
Previous
Next Post »

Blogger templates