Akizungumza na Stori Mix, Nelly Kim alisema: “Nafurahi kufanya kazi na marehemu Kanumba. Nimecheza naye zaidi ya sinema 20 pale kwa Mtitu Game.
Nimejifunza kujiongoza na kuamini katika mambo makubwa, ndiyo maana sasa hivi nasimama na kampuni yangu ya Kasinge Production ambayo inatayarisha na kusambaza filamu.
“Nimesharekodi filamu ya kwanza inayoitwa The Word of God ambayo nimecheza na Kajala, Ben, Kambi na wengineo.
Unajua wasanii hatujitambui, tunakubali kunyonywa wakati tunaweza kujitutumua na kusimamia kazi zetu wenyewe. Hiyo ndiyo siri ya mafanikio ya Kanumba ambayo nataka kuitumia ili kufaidika kwenye sanaa.
Sign up here with your email