Memba wa Klabu ya Bongo Movie Unity wamepambana vilivyo na kufanikiwa kuchangishana Sh. milioni 7 zilizofanikisha shughuli za msiba wa aliyekuwa mwigizaji, prodyuza na mwandishi wa skripti za sinema za Kibongo, Adam Philip Kuambiana.
Chanzo makini kutoka ndani ya klabu hiyo kilieleza kuwa, mastaa hao walipangiana kima cha chini kabisa kila mmoja atoe shilingi elfu hamsini huku wengi wao wakitoa zaidi ya hapo na kufanikiwa kutimiza Sh. milioni 7.
Kuambiana aliyefariki dunia Jumamosi ya wiki iliyopita, alizikwa Jumanne wiki hii katika Makaburi ya Kinondoni, Dar.
Sign up here with your email