MKE WANGU AMBAE ANATUMIA VIDONGE VYA ARV KWA SIRI ANATEMBEA NA MCHUNGAJI WA KANISA LAKE MUME ALALAMIKA


Mwanaume mmoja amemtuhumu mke wake kwa kufanya mapenzi na mwanzilishi wa kanisa la End Time Message Robert Marting Gumbura na waumini wengine saba wa kanisa hilo.
Romeo Ezra jana alimwambia hakimu Tafadzwa Muvhami kuwa mkewe, Octavia, aliambiwa na waumini wenzake akiri kuwa ana mahusiano ya Gumbura. Ezra pia aliiambia mahakama kuwa mkewe amekuwa 
akificha ‘status’ yake ya maambukizi ya virusi vya UKIMWI mpaka pale mtoto wao mmoja alipomwambia yeye kuwa mama yake anatumia vidonge vya ARV. Alifichua hili baada ya mkewe Octavia kutaka kumpeleka mahakamani kuomba ulinzi dhidi yake. Mwanamke huyo, ambaye ni mmoja ya wanawake wanaotuhumiwa kutembea na mchungaji Gumbura alisema Ezra amekuwa akimdhalilisha mbele ya watoto wao.
“Ni muumini wa kanisa la End Time Message na amekuwa akitoka nje ya ndoa na waumini wengine nane wa kanisa hilo akiwemo mchungaji wao, Gumbura, ambaye yuko jela. Gumbura aliniambia kuwa mke wangu alikuwa akimuandikia barua akilalamika kuhusu ndoa yetu. Kwa mujibu wa taratibu za kanisa, hawaruhusiwi kuangalia luninga wala kusikiliza redia lakini amekuwa na DVD nyingi za End Time Message ambazo amekuwa akiziangalia kupitia laptop yake.
“Siku moja nlimuagiza aende akanichotee maji na hapo ndiyo nilipochukua DVD zile na kuziangalia na kutaharuki baada ya kugundua kuwa zilikuwa ni CD za ngono. Nyumba yangu sasa imejaa hizo CD na kila kitu nyumbani kwangu kimepewa jina la kanisa” alisema Ezra.
Hata hivyo, Octavia amekanusha madai ya mumewe. Akasema yeye ni binadamu tu na anaweza akatoka na mwanaume yeyote ambaye anampenda. Mwanamke huyo aliendelea kusema kuwa mumewe huyo alimtelekeza yeye na watoto wake miaka mitano iliyopita, sasa hivi anakuja kunisumbua mbele ya watoto.

Previous
Next Post »

Blogger templates