Balozi wa Libya nchini Tanzania amejiua kwa kujipiga risasi kichwani.
Mwandishi wa BBC mjini Dar es Salaam , John Solombi anasema kuwa balozi
huyo kwa jina Ismail Nwairat, alijipiga risasi Jumanne usiku na kufariki
akiwa anapokea matibabu hospitalini.
Msemaji wa serikali ya Tanzania Arthur Mwambene amethibitisha taarifa
hiyo kuwa balozi huyo alijiua ndani ya makao ya ubalozi wa Libya mjini
Dar es Salaam Jumanne usiku.
Uchunguzi unafanyika kubaini sababu ya kujiua kwa balozi hiyo.
Sign up here with your email