ACHA KUPENDA KUTUHUMU,FANYA UTAFITI UWE NA UHAKIKA.

ACHA KUPENDA KUTUHUMU,FANYA UTAFITI UWE NA UHAKIKA.

Hakika kwenye ndoa au mahusiano kuna mambo mengi ya kujifunza,mojawapo ni kwamba watu wengi wanapenda sana kutuhumu.Mtu hana uhakika,lakini anasema kwa nguvu zote kwamba hiki kiko hivi......kwa namna anavyoongea unaweza kufikiri kwamba anao ushahidi,kunbe hana hata tone.
Anaweza labda akamwona mwenzi wake anaongea kwenye simu au anachati na mtu,hana uhakika anasema kwamba "aaah najua unachati na wanaume au wanawake zako!" Ni kweli inaweza kuwepo ishara zinazosababisha mtu akahisi,lakini ni vizuri zaidi kupata uhakika.
Wapo wanawake,kwamba mwanaume akichelewa kurudi nyumbani,anachojua yeye ni kwamba mwanaume amechelewa kwa wanawake akifanya nao ngono,wakati mwingine mwanaume anaweza asipende kuwahi nyunbani kutokana na mazingira ambayo anatengenezewa hapo nyumbani,kwa mfano akawa hapokewi vizuri na kadhalika.
Pia kuna wanawake wengine wana maneno makali na machafu;kuna wanawake wana maneno ya dharai mno kwa waume zao,hasa pale ambapo labda mume anapokuwa anarudi nyumbani akiwa hana kitu.Furaha ya wanawake wengi ni kuona mwanaune anakuwa ana fedha,arudi nyunbani na zawadi,au fedha,atapewa chochote anachotaka,ndivyo ilivyo kwa wanawake wengi.
Ninachotaka kusititiza hapa ni kwamba si vizuri kupenda kutuhumu ukiwa huna uhakika.Mwanamke au mwanaume hauna uhakika naye kwamba anafanya ngono na fulani kisha unamtuhumu kwamba anafanya naye,kwa ambaye akili yake haijatulia,anaweza kusema bora sasa kufanya kweli.
Pia katika ndoa au mahusiano mengi watu wamekuwa maarufu sana wa kutaka mazuri kwa wenzi wao,lakini wao hawana muda wa kufanya mazuri.Ni kwamba baada ya mumeo kurejea kutoka kazini au kokote,jitahidi kumpokea katika hali nzuri kwa maana kwamba onyesha sura ya uchangamfu,zaidi ya yote hakikisha unakuwa mwenye kuvutia kuanzia mavazi na mwili wako kwa ujumla hasa unatakiwa kuoga na kutumia manukato mazuri.
*unatakiwa utambue kwamba unapokutana na mumeo kwa mara ya kwanza akitokea katika mihangaiko ya maisha au safarini,anza kwanza kwa habari nzuri....baada ya muda akiwa ametulia ndipo uanze kumwambia habari mbaya Maana kuna wengine utasikia wanawapokea waume zao kwa habari mbaya "mfanyakazi wa ndani leo amenikwaza sana,nimemtuma maji kaniambia kachoka...kanikwaza sana natamani atoke" Ndugu yangu ni vyema kuwa na hekima kwa kuangalia maneno gani ya kuanza nayo...matatizo yapo,kwa maana hiyo unapaswa kuyafahamu na kuchukua hatua za maana.Ni vizuri kumpokea mumeo kwa maneno yaliyojaa upendo,mapenzi na shauku ya kuwa pamoja nae.
*Jambo lingine ambalo wanawake wengi wanakosea ni kuhusu chakula..wengi huwa wanapika wanavyotaka wao..wala hana muda wa kumuuliza mumewe leo ungependa nipike nini.Ndugu yangu nje ya kutayarisha kwa wakati,pia unapaswa kupika chakula kwa wakati.
Lingine la msingi,acha kutumia kauli za hasira kama walivyo baadhi ya wanawake,maana ukiuliza hiki utaambiwa kwa ukali au kwa mkato.

MAMBO MENGINE YA MSINGI.
Previous
Next Post »

Blogger templates