Ndosi ya ukweli: Radamel Falcao (katikati) akipiga kichwa murua na kuifungia Monaco bao la kuongoza.
ASERNAL walifungwa bao 1-0 na Monaco na kupoteza kombe la Emirates, ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya msimu mpya wa ligi kuu soka nchini England.
Hata hivyo dhahiri shahiri mwamuzi wa mechi hiyo Martin Atkinson aliwanyima washika bunduki penalti ya wazi.
Bao pekee la ushindi kwa Monaco, lilifungwa na mshambuliaji mwenye thamani ya paundi milioni 53, Radamel Falcao.
Bao hilo la kichwa ni la kwanza kwa Falcao tangu apate majeraha ya goti mwezi januari mwaka huu.

Mabeki wa Asernal hawakuwa makini kumkaba Falcao.

Shangwe: Falcao (wa pili kushoto) akipongezwa na wenzake baada ya kuifungia bao la kuongoza

Si kuoneana huku?: Chuba Akpom akichukua mpira na kumpiga chenga kipa wa Monaco, Daniel Subasic

Dhahiri ndani: Akpom akiangushwa ndani ya eneo la hatari na kipa wa Monaco

Licha ya tukio hili kutokea eneo la hatari, mwamuzi alitoa adhabu ndogo

Penalti: Mwamuzi Martin Atkinson akionesha ishara ya penati baada ya Akpom kuangushwa

Kabadili moyo wake: Ghafla Atkinson alibadili maamuzi na kutoa adhabu ndogo baada ya kushauriwa na mwamuzi msaidizi

Angalau Umefurahi eeeh?: Atkinson na msaidizi wake wakitabasamu wakati wanatoka uwanjani baada ya mechi kumalizika

Wee vipi?: Mathieu Flamini (katikati) akipinga maamuzi ya refa
Sign up here with your email