miongoni mwa jamii kwamba imekuaje
vijana wa kiume wamekuwa ni waongo
sana hasa linapokuja swala la kuoa? Kwa
kadiri siku zinavyozidi kwenda ndivyo
ambavyo idadi ya wanaume wanaoogopa
kuoa inazidi kuongezeka. Utakuta
wapenzi wanaambiana kwamba
wanapendana na kuahidiana kuwa
wataoana, lakini kitakachotokea baada ya
hapo ni mwanaume kuanza kupiga
chenga kwa visingizio lukuki.
Kwa nini hali hiyo hutokea?
Ukweli ni kwamba hakuna jibu la moja
kwa moja juu ya tatizo hilo, lakini yapo
mambo ambayo yanaweza kutupa
angalau tafakuri. Nitajaribu kudadavua
baadhi ya sababu zinazowafanya
wanaume siku hizi kukwepa kuingia
katika taasisi ya ndoa:
1 Ukosefu wa mtu wa kumchukulia
kama mfano:
Hapa nawazungumzia wale watoto wa
kiume waliolelewa malezi ya upande
mmoja yaani walilelewa na mama peke
yao. Sina maana ya kudharau au kutweza
malezi ya mama, la hasha, lakini ni vyema
mkafahamu kwamba kuwa na baba asiye
na malezi mazuri si sawa na kutokuwa na
baba. Na ndio maana nikasema ukosefu
wa mtu wa kumchukulia kama mfano.
Achilia mbali aina ya malezi atakayoyapata
kwa familia yawe mazuri au mabaya lakini
lazima kutakuwa na tabia za kiume
zitakazoakisi malezi ya mtoto wa kiume
katika familia husika. Watoto waliolelewa
na mama peke yao kuna kitu huwa
wanakosa, kwani wanakuwa hawana mtu
wa kumchukulia kama mfano kwa upande
wa jinsia ya kiume na hapo ndipo hujikuta
wakijifunza wenyewe namna ya kuongea
na kutenda kama wanaume kwa sababu
katika makuzi yao hawakupata fursa ya
kuwa karibu na baba zao. Kwa kuwa siku
hizi kuna kundi kubwa la kina mama
ambao wamejikuta wakiachiwa mzigo wa
malezi ya watoto, baada ya aidha
kuachwa na waume zao au kuzalishwa na
kutelekezwa (Single mothers), na hapo
ndipo tunaposhuhudia mtoto wa kiume
anapokua kwa umri na kimo huku akiwa
hana mtu wa kumuangalia kama mfano
wa mume anavyotakiwa kuwa katika
familia zaidi ya kujifunza mambo hayo
kupitia katika TV, senema au miziki.
Wanaume waliopitia malezi ya aina hii
huchelewa sana kuoa kwani huyaangalia
maisha ya ndoa kwa namna ya kujaribu
na ndipo hapo wengi huishia kuishi
kinyumba na wanawake kwa ajili ya
kutaka kujifunza namna ya maisha ya
ndoa yanavyotakiwa kuwa na ndio
sababu huchukua muda mrefu kufanya
maamuzi. Na mara nyingi huishia
kubadilisha wanawake kutokana na
kutokuwa na uhakika wa kile
wanachokitafuta.
2 Mgogoro wa kiuchumi:
Kuna kundi kubwa la vijana siku hizi
hawana ajira au hawana uhakika na
kipato. Ukweli ni kwamba hakuna
mwanaume atakayependa kujiingiza
kwenye ndoa wakati hana kazi au hana
uhakika na kipato chake. Na hiyo ni
kutokana na wanawake wengi siku hizi
kuonekana kujali zaidi wanaume wenye
uhakika na kipato. Hii misemo ya
wanawake ya kebehi dhidi ya wanaume
wasio na ajira au kipato, kama vile
"mwanaume suruale" ina mchango
mkubwa sana katika kuwafanya
wanaume kukwepa kuoa iwapo hawana
ajira au hawana uhakika na kipato chao.
3 Wanawake wengi kuwa na kiwango
cha elimu ya juu:
Siku hizi wanawake wengi wameibuka
katika kutafuta elimu ya juu kwa juhudi
kubwa. Idadi ya wanawake wanaojiunga
na vyuo vikuu ni wengi tofauti na
ilivyokuwa zamani. Na hiyo ni kutokana na
wazazi wengi kubadili mtazamo wao juu
ya mtoto wa kike. Zamani mtoto wa kike
alichukuliwa kama kitega uchumi. Kwa
maeneo ya vijijini na katika familia
masikini, watoto wa kike walikuwa
wanatazamwa kama, 'biashara ya kesho'
ambapo watauzwa kwa njia ya mahari.
Kwa hiyo thamani yao ilikuwa ni kuolewa,
ni ile ya kibidhaa na sio kibinadamu.
Lakini tofauti na zamani siku hizi hata kule
vijijini kumekuwa na mwamko mkubwa
sana wa kumsomesha mtoto wa kike hadi
elimu ya juu. Kutokana na mwamko huo
wanawake wengi wamejikuta wakiona
elimu kama kimbilio pekee la kuepukana
na mfumo dume. Mwanamke gani
atakubali kunyanyaswa na mwanaume
akiwa na elimu yake na labda pia akiwa
na kazi yake yenye mshahara na
marupurupu ya kutosha, naamini
watakuwa ni wachache sana ambao
hawajiamini au waliathiriwa na malezi.
Kwa upande wa wanaume nao,
wamejikuta wakiwaogopa wanawake
hawa wenye elimu ya juu kwa hofu ya
kuzidiwa kipato na labda kukosa sauti
kama mwanaume na hiyo inatokana na
ego tu.
4 Wanaume huwaona wanawake kama
tishio wanapokuwa na mafanikio
makubwa kifedha:
Inaweza kutokea mwanaume anaweza
kuwa na uhusiano na mwanamke ambaye
labda tu nisema ni mbangaizaji. Wakati
huo anaweza kuahidi kufunga ndoa na
mwanamke huyo, lakini iwapo itatokea
mwanamke huyo akapata mafanikio
kibiashara na kuinuka kifedha. Kama
mwanamke asipokuwa makini anaweza
kusababisha mwanaume huyo akaingia
mitini. Sababu kubwa hapo inaweza kuwa
ni hofu ya kuogopa kuongozwa na
mwanamke. Kumbuka kwamba mfumo
dume bado umetawala vichwani mwa
wanaume wengi kutokana na malezi.
Mwanaume asiyejiamini ni vigumu sana
kwake kuoa mwanamke aliyemzidi kipato.
Kwa sababu akifanyiwa jambo dogo tu,
inakuwa kama ametoneshwa. Atahisi
kutaka kutawaliwa na mwanamke huyo.
Jambo ambalo wanawake wanatakiwa
kulifahamu ni kwamba kila mwanaume
anataka kutambuliwa na kuheshimiwa
kama shujaa kabla ya kumfuata msichana.
Iwapo utakuwa umesimama iwe ni
kifedha au kielimu pale unapotafuta
kupata mwenza, inabidi ujishushe sana la
sivyo utadoda.
5 Wanaume wengi siku hizi wana hofu
ya majukumu, hasa ya kulea watoto:
Kutokana na malezi yao au kile
wanachokijua kuhusu watoto, baadhi ya
vijana huamini kwamba, kulea watoto ni
jambo gumu sana. Lakini wengine
wanaamini kwamba, hata mke anapaswa
kulelewa kama ilivyo kwa mtoto. Hivyo
wanaamua kutafuta kwanza uwezo
ambao haupatikani kiurahisi. Kuna
wengine, ambao wamefundishwa au
kuelekezwa na mila na desturi zao
kwamba, kabla hawajaoa, ni lazima wawe
na nyumba kwanza, tena kwao. Kwa hiyo,
hawa hadi waje wapate uwezo wa fedha
wanakuwa wameshachelewa.
6 Kuna baadhi ya wanaume, maisha bila
ya ndoa wanayaona kuwa ndiyo bora
kuliko yale ya ndoa:
Kuna baadhi ya wanawake hujirahisisha
sana kwa wanaume. Siku hizi ni jambo la
kawaida sana kukuta mwanaume anaishi
na mwanamke bila ndoa, wenyewe
wanaita Trial Marriage. Na hapo ndipo
unapokuta wanaume hawaoni tena
umuhimu wa kuoa. Sasa kama
mwanamke anaweza tu kuishi na
mwanaume bila ya ndoa na mwanaume
huyo akapata huduma zote kutoka kwa
mwanamke huyo, unadhani ni kitu gani
kitamvuta kufunga ndoa. Jambo lingine ni
ile dhana kwamba maana ya ndoa ni
tendo la ndoa. Siku hizi wanaume wengi
wamejikuta wakiwa hawahitaji tena kuoa
kwa sababu tendo hilo linapatikana
kiurahisi tofauti na zamani. Siku hizi
inawezekana kabisa kumtongoza binti leo
na kupata tendo siku hiyo hiyo….. Na hapa
siwazungumzii makahaba.
Nawazungumzia mabinti zetu ambao
wengine ukiwaona ni watu wa
kuheshimiwa ukiwaangalia kwa nje lakini
kwa ndani hawana lolote, vijana wa siku
hizi wenyewe huwaita maharage ya
Mbeya.
Kuna sababu nyingi zinazotajwa
kusababisha wanaume siku hizi kujivuta
sana katika kufanya maamuzi ya kutafuta
mwenza. Lakini hizo chache nilizozitaja
Sign up here with your email