REAL MADRID MABINGWA SUPER CUP ULAYA

Wafalme wa Ulaya; Wachezaji wa Real Madrid wakifurahia na taji lao la Super Cup ya UEFA leo
MABAO mawili ya Cristiano Ronaldo, moja kila kipindi yametosha kuipa Real Madrid ushindi wa 2-0 dhidi ya Sevilla, zote za Hispania Uwanja wa Cardiff City mjini Cardiff na kutwaa Super Cup ya UEFA.Sifa zimuendee nyota wa Wales, Gareth Bale aling'ara akicheza kwenye ardhi ya nyumbani na kutoa mchango mkubwa katika ushimdi huo. Ronaldo alifunga bao la kwanza dakika ya 30 na la pili dakika ya 49. 
Kikosi cha Real Madrid kilikuwa: Casillas, Carvajal, Pepe, Sergio Ramos, Fabio Coentrao, Kroos, Rodriguez, Modric, Bale, Benzema, Ronaldo. 
Sevilla: Beto, Coke, Pareja, Fazio, Fernando Navarro, Alex Vidal, Krychowiak, Carrico, Vitolo, Suarez, Bacca
Previous
Next Post »

Blogger templates