“Mama Kanumba ni rafiki yangu wa ukweli, ana mapenzi mazito sana kwangu amekuwa mstari wa mbele kunishauri na kunipa mwongozo wa maisha ni nini na wapi nilipokosea na natakiwa kufanya nini ili kuwa na maisha yaliyonyooka,” anasema mwigizaji huyo anayetamba na filamu ya Foolish Age. Lulu mwenye miaka 19, anasema haikuwa rahisi kwake kufikiria kutulia kiuhusiano ila amepewa mwongozo bora unaomfanya afikirie kufanya hivyo kwa sasa. “Mimi ni binti na kama ujuavyo nina mapenzi yangu moyoni, si kazi rahisi kuamua kwa sasa lakini nimepewa mwongozo bora na kuona nini natakiwa kufanya. Kama binti napaswa kuzingatia maadili, mimi ni kioo cha jamii, inafika hatua inabidi niishi katika maadili hilo ndilo ninalolifanya sasa.” Anasema wazazi wake wamempa baraka zote kuhusu uhusiano wake wa sasa: “Wazazi wangu sasa wanafahamu kwamba nimepata mchumba, kwa kweli wamenipa baraka zao zote, pande zote hata Mama Kanumba. Nimekua sasa na mimi nina uamuzi wangu, ni vema kuangalia ninataka nini lakini kikubwa wananishauri.” Anasema wazazi wake hawakubali kila anachokitaka: “Sina wazazi wa kukubali kila ninachokitaka ila nina wazazi waelewa, wenye kuangalia jambo kabla hawajaniambia sasa unaweza kuendelea, mama yangu ni mkali sana, hana mchezo hasa pale anapoona kwamba nayumba kimaisha,” anasema Lulu. Kuhusu tetesi zilizoenea kwamba ana uhusiano na msanii wa hip hop Young Dee, Lulu alikana na kusisitiza kwamba hajawahi hata kuwa na ukaribu na msanii huyo. “Nashangaa taarifa hizo watu wanazitoa wapi na mpaka leo nashangazwa na uvumi ulioenea kwamba tulifumaniwa, usiku ule nilikuwa sehemu nyingine tofauti kabisa, ukweli ni kwamba sijawahi kuwa na ukaribu na Young Dee, wala hata kumfikiria kama ninaweza kuwa na uhusiano naye. Bado, hatulingani kwa kweli,” anasema.
Sign up here with your email