Linex akanusha kuwa na uhusiano wa mapenzi na Agnes Masogange, …”Sina haraka ya kuwa na mpenzi”

linex
Linex Sunday Mjeda, ambaye hivi karibuni ameonekana kwenye picha kadhaa akipoz na video Queen maarufu Tanzania, Agnes Gerald (Masogange), amekanusha kuwa na uhusiano wa mapenzi na mrembo huyo.
 

Kupitia akaunti yake ya Facebook, mkali huyo wa ‘Kimugina’ ameonesha kusikitishwa na habari iliyoandikwa na tovuti moja kuwa yeye na Agnes wako kwenye mapenzi mazito.
 

“Ni kweli watu wa blog mnapush sana kazi zetu but nimesikitishwa na habari hii iliyoandikwa na blog kadhaa mtasababisha tutashindwa ata kukaa na Dada zetu au marafiki zetu Uliza b4 Hujaandika ujinga am single na sina haraka ya kua na mpenzi.” Ameandika kwenye Facebook.
 

Wikendi hii, Linex alipost picha mbili Instagram akiwa na mrembo huyo, moja wakiwa wamepoz ufukweni, na nyingine akiwa naye katika mechi ya mpira wa kikapu kati ya timu za madirector wa video za muziki Tanzania, Adam Juma na Karaban. ——Times 100.5 FM
Previous
Next Post »

Blogger templates