UNATAKA KUISHI KIMAPENZI? CHUKUA MUONGOZO HUU!

https://www.facebook.com/theclicktzNi elimu ambayo kila mtu anatakiwa kuwa nayo kwamba kutofautisha maeneo ni jambo la busara. Kwamba sura yako iwe nyingine unapokutana na watu wa mitaani, itofautiane unapokuwa na wazazi, vivyo hivyo pale ambapo upo sehemu ‘spesho’ na mwenzi wako. 
Lazima uwe unabadilika kama kinyonga. Ukiwa kazini mbele ya watu unaowaongoza unazungumza kwa sauti ya amri, lakini hiyo hupaswi kuitumia unapokuwa na wazazi wako. Unaongea kwa sauti kali ya kuamrisha mbele ya baba yako, hiyo adabu umefundishwa wapi?
Kuna lugha ya kuzungumza ukiwa na mwenzi wako. Ni mwiko kutoa sauti ya kuamrisha. Ni vizuri kumnyenyekea lakini si katika kiwango ambacho kitakufanya uonekane una kasoro za kisaikolojia. Tawile kwa kila linalosemwa na mpenzi wako hairuhusiwi, unatakiwa kuweka mbele hisia zako.
Upole kupitiliza hauna maana kwamba wewe ni mpenzi sahihi. Eti, utaonekana una nidhamu na unamsikiliza vizuri mwenzio, la hasha! Utatambulika kuwa mtu hai kulingana na jinsi akili yako inavyofanya kazi. Namna hisia zako zinavyoonesha uhai unapogushwa na matukio mbalimbali ndivyo na ubinadamu wako unavyosomeka.
Unahoji mambo kwa sauti yenye ujazo wa kutosha, unachukia pale unapoona mambo hayajaenda sawa, unaumia pale unapotendwa na unafurahi mipango inapokuwa chanya. Hii ndiyo mantiki ya kukutaka uwe na akili hai. Itashangaza umepata habari kwamba mwenzi wako yupo gesti na mpenzi mwingine halafu utabasamu.
Sumu hatari inayosababisha mmomonyoko wa ndoa au uhusiano wa kimapenzi kwa watu wengi ni kushindwa kujipanga kimaeneo. Ratiba za ofisini kuingiza nyumbani. Marafiki kuathiri taratibu za mapenzi yenu, ingawa kila kitu kina umuhimu wake kulingana na wakati husika.
Umeudhiwa na wafanyakazi wenzako kazini, unatakiwa kuweka hekima mbele. Unarudi nyumbani ukiwa na imani kwamba huko utakutana na mwenzi wako na ndiye mfariji wako. Kichwa kizito, basi mueleze mwenzio ajue kinachokusibu kuliko kumpa majibu ya mkato. Itakuharibia badala ya kukusaidia.
Ukirudi umenuna, mwenzio anakusemesha umekunja ndita ni kosa kubwa. Na kama utashindwa kujirekebisha inaweza kukusababishia kasoro za kimaumbile. Utaonekana mkorofi kumbe ni kosa la kutokujipanga. Haiwezekani kibano ulichopewa ofisini na bosi wako, hasira uzimalizie nyumbani.
Hii ndiyo sababu ya kukutaka ujifunze kuweka maudhi ya pembeni kando unapokuwa na mwenzi wako. Unapovuka kizingiti cha mlango, hakikisha hasira zote unaziacha hapo ili unapoingia ndani kichwa chako kiwe chepesi kupokea yaliyomo ndani ya nyumba.
Inahitaji hekima za hali ya juu kusahau maudhi ya nje haraka, kwani wengi wamekuwa shubiri kwa wapenzi wao. Anaingia ndani, mwenzake anampokea kwa bashasha lakini badala ya kumpokea, anamsukuma! Kitu kidogo anafoka: “Usinitibue, kichwa changu hakipo sawa leo.”
Nimeeleza kuwa inahitaji mtu mwenye hekima ya kiwango cha juu kuweza kuepuka hasira za pembeni anapokuwa na mwenzi wake. Ni moyo wa kishujaa kweli, kwani wengi moto wan je huuwasha ndani mpaka nyumba inashindwa kukalika.
Inawezekana kiwango cha uvumilivu ni kidogo, kwahiyo ni ngumu kutenganisha maudhi kwa haraka, hivyo hapa chini kuna njia sita ambazo zinaweza kukusaidia kukabiliana na hali hiyo pale yanapokufika.
- globalpublishers
Previous
Next Post »

Blogger templates