breaking news:HOSPITALI YA TMJ YANUSURIKA KUUNGUA JIONEE PICHA


 Baadhi ya wagonjwa wakiwa wametolewa hospitali ya TMJ baada ya nyumba ya jirani kuwaka moto. Walitolewa wodini kwa tahadhari.

 Mgonjwa alitolewa nje ya wodi na jamaa yake.

 Askari wakiwa katika hekaheka za kuzima moto.
 Mama huyu mgonjwa akitolewa wodini na ndugu yake baada ya nyumba jirani kuwaka moto.

 Gari la Zima Moto likiwa nje ya hospitali ya TMJ.

 
Mhudumu akimtoa nje ya wodi mgonjwa, kwa tahadhari baada ya nyumba jirani na hospitali hiyo kuwaka moto.

 
Kikosi cha Kuzima Moto kikizima moto nyumba jirani na Hospital ya TMJ iliyopo Mikocheni Dar es Salaam muda huu na watu kudhani kuwa iliyokuwa ikiungua ni hospitali.

 
Wagonjwa wakitolewa nje na manesi wa Hospital ya TMJ baada ya nyumba jirani kuwaka moto.

Hospital ya TMJ iliyopo Mikocheni Dar es Salaam ilizushiwa kuwaka moto baada ya nyumba jirani kulipuka moto, hali iliyosababisha hekaheka kwa wafanyakazi wa hospitali hiyo ya kuwatoa nje wagonjwa kwa tahadhari.
Tahadhari hiyo ilichukuliwa kutokana na wasiwasi kuwa moto huo ungeweza kuvuka na kuingia hospitali lakini ulidhibitiwa na kikosi cha zima moto na kuishia katika nyumba hiyo ya jirani


Read more: http://www.vitukovyamtaanews.com/2014/04/breaking-newshospitali-ya-tmj.html#ixzz2xTSW4RbO
Previous
Next Post »

Blogger templates