Leo tunakuletea list ya ma star watano wanaoongoza katika social network, listi hii inakusanywa na mtandao wa swahilitz kuanzia kwenye facebook, twitter na instagram ni msanii gani anaongoza kati ya wote hapa bongo. Vigezo vilivyotumika kuwapata top 5 hii ni idadi ya juma ya mashabiki wa wasanii hawa katika mitandao yote mitatu na kisha kupata wastani wa mashabiki
Well wacha tuanze list hii tukianza na namba moja hadi 5, unadhani ni nani kaongoza katika list hii fatilia hapa..
Well wacha tuanze list hii tukianza na namba moja hadi 5, unadhani ni nani kaongoza katika list hii fatilia hapa..
1. Lady Jay Dee aka Komando aka Anaconda.
Lady Jay Dee
Judith Wambula likiwa ndiyo jina lake halisi la kwenye kitambulisho ila jina la kisanii anajulikana kama Lady Jay Dee, ni msanii wa kike aliyetamba katika game karibia miaka 15 mpaka sasa tangu aanze muziki na ndiye star anayeongoza kuwa na mashabiki wengi zaidi katika social network. katika ukurasa wake wa facebook Lady Jay Dee ana like zaidi ya 262,583 huku katika akaundi yake ya twitter ana followers zaidi ya 76k na instagram ana follower 27,520 huku akiwa na wastani wa mashabiki 122034.3 katika mitandao yote mitatu ya kijamii
2, Diamond Platnumz aka Dangote
Diamond Platnumz
Jina la kwenye ID ni Naseeb Abdul ila linalompa kula ni Diamond Platunumz, kwa upande wa muziki wa bongo fleva huyu ndiye msanii anayelipwa Pesa nyingi zaidi kwa kila show anayofanya iwe ndani au nje ya Bongo na kadri siku zinavyozidi kwenda anazidi kujiongezea umaarufu na umaarufu unapanda zaidi kutokana na mahusiano ya kimapenzi aliyonayo na mtoto wa marehemu mzee Sepetu, Diamond anashika nafasi ya pili akiwa na likes 164,665 katika facebook na twitter ana followers zaidi ya 62.9k, huku instagram akiwa na followers zaidi ya 101k huku instagram akiwa na followers 43,678 huku akiwa na wasani wa mashabiki 109521.7 katika mitandao yote mitatu ya ya kijamii
3. Masanja Mkandamizaji aka Mchungaji
Masanja Mkandamizaji
Jina la kwenye kitambulisho ni Emanuel Mgaya ila anajulikana kama Masanja Mkandamizaji, umaarufu wake ulianza alipokuwa akifanya kipindi cha comedy katika kituo cha channel 5 na baadae kuhamia TBC1 katika kipindi chote hicho Masanja anahesabika kuwa ni miongoni mwa wachekeshaji wakubwa zaidi hapa Tanzania. Masanja anashika nafasi ya tatu katika countdown yetu huku akiwa na likes 200,177 katika ukurasa wake wa Facebook huku katika twitter akiwa na follower zaidi ya 91.1k na instagram ana follower 16,448 huku akiwa na wasani wa mashabiki 102575 katika mitandao yote mitatu ya kijamii
4. Millard Ayo aka Mtu wangu wa Nguvu
Millard Ayo
Siku baada ya siku jina lake linazidi kukuwa hasa akiwa ndiye kijana anayewavutia watu wengi wa kila lika kwa namna ya utangazaji wake na muonekano wake kwa ujumla. Millard Ayo ni mtangazaji wa Clouds anayekuwa na kipindi kila siku za wiki kuanzia saa 1 kamili hadi saa3 usiku akiwa anahesabu habari 10 za moto za ndani na nje ya bongo. Millard Ayo anashika nafasi ya 4 akiwa na jumla ya likes 169,298 katika facebook na twitter ana followers zaidi ya 87.7k, huku instagram akiwa na followers 43,678 huku akiwa na wasani wa mashabiki 100225.3 katika mitandao yote mitatu ya kijamii
5.Wema Sepetu aka Madame
WEMA SEPETU
Jina la wema limekuwa gumzo kila kukicha katika social media na kwenye magazeti ya udaku kwani kila siku lazima awepo katika magazeti hayo. Wema sepetu ambaye kwa sasa ni mpenzi wa mwanamziki Diamond Platnumz. Wema anajumla ya likes 82,651 kwenye facebook na twitter ana followers zaidi ya 65.9k huku instagram akiwa na followers 88,683 huku akiwa na wasani wa mashabiki 79,078 katika mitandao yote mitatu ya kijamii
Sign up here with your email