Watu watatu waliofahamika kwa majina ya Msagala, Jacob na Mhando wakazi wa Bunju jijini Dar es Salaam wamefariki dunia.
Shughuli ya uokoaji ikiendelea.
Waokoaji baada ya kugundua mwili ulipo.
Watu waliofika eneo la tukio kuwatambua marehemu.
Watu watatu waliofahamika kwa majina ya Msagala, Jacob na Mhando wakazi wa Bunju jijini Dar es Salaam mchana wa leo wamefariki dunia baada ya kufukiwa na kifusi wakati wakichimba kokoto kwenye machimbo ya Mtanzania mwenye asili ya Kiasia aliyefahamika kwa jina la Kara Arjan yaliyopo Bunju-Mbweni jijini.
Habari zilizopatikana eneo la tukio zilisema kuwa machimbo hayo yalishapigwa marufuku kutokana na watendaji wake kufanya kazi katika mazingira hatarishi. Wachimbaji hao wakiwa kazini, sehemu ya machimbo hayo iliporomoka na kuwafukia.
Sign up here with your email