P. DIDDY ATUNUKIWA SHAHADA YA HESHIMA CHUO KIKUU CHA HOWARD

Ni furaha tupu siku P. Diddy alipotunukiwa shahada ya heshima katika Chuo Kikuu cha Howard jana jijini Washington DC.
Akiwa katika furaha kubwa mbele ya jumuia ya chuo hicho.
  Diddy akiwahutubia wanajumuia wa chuo hicho.
Diddy akipozi na mwanamuziki Mary J. Blige chuoni hapo.
Mwanamuziki huyo tajiri akionyesha moja ya hati zake muhimu.
Akiwa jukwaani (kushoto) wakati akisubiri kuwahutubia wanajumuia wa chuo hicho.
MWANAMUZIKI wa Marekani, P. Diddy ambaye jina lake halisi ni Sean Combs, ametunukiwa shahada ya heshima jana (Jumamosi) katika Chuo Kikuu cha Howard cha jijini Washington DC. 
Mwanamuziki huyo wa mtindo wa hip-hop aliwahi kusoma katika chuo hicho kwa miaka mwili kabla ya kuondoka na kwenda kujikita katika muziki.
Akihutubia wanafunzi chuoni hapo, mwanamuziki huyo mwenye umri wa miaka 44 ambaye amerudia tena jina lake la Puff Daddy,  alisema kwamba wasomi ndiyo huleta mabadiliko duniani kutokana na nguvu za ndoto na mategemeo yao.
“Chuo Kikuu cha Howard hakikubadili tu maisha yangu, bali kiliingia katika roho, moyo na mwili wangu wote,” alisema katika hotuba yake.
Mwanamuziki huyo ambaye pia ni mbunifu wa mitindo na sasa ni ‘doctor’, kwa mujibu wa jarida la Forbes, ni tajiri zaidi wa wanamuziki wote wa mtindo wa hip-hop akimiliki dola milioni 700.
Pamoja na vituko vingi vya msanii huyo ambaye aliwahi kuwa mshikaji wa mwanamuziki Jennifer Lopez wa Marekani, amekuwa akiwababaisha mashabiki kwa kubadili kila mara majina yake ambapo sasa amerudia jina la Puff Daddy aliloliacha na kuanza kutumia lile la P. Diddy mnamo mwaka 2001 kabla ya kuchukua tena jina la Diddy pekee ambapo sasa amesema hajawahi kubadili jina lake ambalo ni Puff Daddy.
Previous
Next Post »

Blogger templates