"Ni muda mrefu nimekuwa nikifuatilia mienendo ya mume wangu kutokana na tabia yake kubadilika sana siku za hivi karibuni, nikabaini kuwa kuna msichana anawasiliana naye kwa kutumiana meseji za mapenzi, sikuwa na haraka nikaamua kufanya uchunguzi wangu kimyakimya"
"Wiki iliyopita mume wangu akiwa amekwenda kuoga akasahau kuzima simu yake,na siyo kawaida yake kuacha simu yake bila kuizima,mara meseji ikaingia,nikaangalia nikaona jina la mtumaji amesevu Lulu, moyo ukalipuka"
Ndivyo alivyoanza kuongea mama mmoja wa makamo anayefanyakazi katika ofisi moja nyeti katikati ya jiji la Dar alipokuja kuongea na mwandishi wetu wiki iliyopita baada ya ndoa yake kuingiliwa na mdudu mbaya....
Akiongea kwa masikitiko makubwa, mama huyo ambaye hakupenda kutaja jina lake kutokana na unyeti wa kazi anayoifanya, alidai kuwa msichana huyo anayetaka kuiharibu ndoa yake yenye miaka 25 jina lake ni Elizabeth Michael....
Mama huyo alidai kuwa jina hilo alilibaini baada ya kukuta meseji za mapenzi kwenye simu ya mume wake na yeye kuamua kuifuatilia namba hiyo kwa kufanya kama anataka kumtumia pesa msichana huyo na kukugundua jina hilo....
Akiongea kwa upole, mama huyo alidai kuwa katika simu ya mume wake, jina la mtumaji lilikuwa Lulu, lakini alipofanya uchunguzi wake wa kujifanya kama anatuma pesa kwa namba ya msichana huyo ndipo alipobaini kuwa mmiliki wa namba hiyo ni Elizabeth Michael...
Mwandishi alimuuliza mama huyo kama anadhani kuwa msichana huyo anayetaka kuiharibu ndoa yake ni muigizaji maarufu wa filamu hapa nchini Elizabeth Michael "Lulu", lakini alikataa kuthibitisha hilo kwa madai kuwa tangu siku hiyo namba ya binti huyo imekuwa haipatikani....
"Baada ya kugundua siku ile , nilichukua simu yake na kutaka kuwasiliana naye ili niweze kumuonya mwenyewe kimyakimya kwa wakati wangu, wala sikuwa na lengo la kuja kwenye vyombi vya habari , lakini sikuwahi kumpata hewani tena kila nilipojaribu kumpigia"Alisema na kuongeza:
"Huenda mume wangu alishtikia kuwa nimeona ujumbe ule, kwa sababu mimi nilipoisoma meseji ile sikuifuta, ili akiona meseji imesomwa aelewe nimeshajua kila kitu, pengine ndiye aliyemwambia binti huyo abadili namba yake"
Mwandishi alimuomba mama huyo ampatie namba ya huyo msichana ili kuweza kujua kama ni Lulu muigizaji ama siyo ( mwandishi anazijua namba zote za Lulu ), lakini namba hiyo ni tofauti na anazotumia Lulu Mwenyewe....
Mwandishi alipojaribu kama kumtumia pesa msichana huyo, jina lililotokeza ni Elizabeth Michael, na alipojaribu kuipiga namba hiyo ilikuwa haipatikani hewani....
Juhudi za kumsaka Lulu ili kuona kama anaitambua namba hiyo hazikuzaa matunda kutokana na namba zake mbili kutopatikana na nyingine ikiita bila kupokelewa....
Angalizo:
Baadhi ya wasichana wa mjini wamekuwa wakitumia majina ya wasanii maarufu katika nyendo zao ili kuwatapeli watu. Miongoni mwa njia wanazotumia ni pamoja na kujisajili kwenye mitandao ya kijamii kwa majina ya watu maarufu ili kuwatapeli watu.
Source: Gazeti la Visa
Source: Gazeti la Visa
Sign up here with your email