
WENYEJI Brazil leo Alhamisi watakuwa na kibarua pevu cha kuhakikisha wanaanza vyema michuano ya Kombe la Dunia ambapo wanatarajiwa kufungua pazia kwa kumenyana na timu ya taifa ya Croatia kwenye Uwanja wa Rio de Janeiro mjini hapa.

Mara ya mwisho timu hizo zilipokutana kwenye michuano ya Kombe la Dunia mwaka 2006 iliyofanyika nchini Ujerumani, Brazil iliichapa Croatia bao 1-0 lililotupiwa kimiani na kiungo Ricardo Kaka ambaye mwaka huu hajaitwa katika timu hiyo.

Kwa upande wa Croatia kupitia kwa kocha wao Niko amesema kikosi chake hakitapaki basi kwenye mchezo wa leo ambao wenyeji wanapewa nafasi kubwa ya kushinda.

Wachezaji tegemeo Croatia: Darijo Srna, Dejan Lovren, Vedran Corluka, Danijel Pranjic, Luka Modric, Mario Mandzukic, Ivica Olic, Eduardo
Sign up here with your email