Vikosi vya serikali Somalia vimefanikiwa
kuidhibiti upya ikulu ya rais katika mji
mkuu Mogadishu baada ya hapo awali
wapiganaji wa kiislamu kuishambulia.
Maafisa wanasema washambuliaji wapatao watano
kutoka kundi la al-Shabab waliuawa walipoingia
katika eneo la ikulu hiyo.Washambuliaji hao wanadaiwa
kulipua bomu lililotegwa kwenye gari karibu na langu kuu
la Ikulu hiyo.
Waziri wa habari na mawasiliano wa Somalia Mustaf
Dhuhulow ameambia BBC kuwa tayari mmoja
wa washambuliaji hao amekamatwa na anahojiwa na
polisi.
Waziri Mustaf amesema, '' Walishambulia ikulu ya rais
saa za jioni. Alikuwa watu washambuliaji watatu
pamoja na dereva wao. Washambuliaji hao waliuawa
lakini dereva wao alipata majeraha madogo na anazuiliwa
na polisi na kuhojiwa. Walijaribu kuvamia Villa Somalia
lakini wakakomeshwa. Tutawapa maelezo zaidi baadaye.
Na tutaweza kutoa maelezo zaidi kwa raia wa Somalia na
dunia nzima.''
Hii ni mara ya pili kwa Al Shabaab kuvamia ikulu ya
rais mjini Mogadishu mwaka huu japo mara ya
kwanza walifanikiwa kuingia ndani.Rais Hassan
Sheikh Mohamoud hakuwepo wakati wa shambulio
hilo.
Kundi la wapiganaji wa kiislamu Al shabaab limefukuzwa
kutoka mjini Mogadishu tangu mwaka wa 2011 lakini
limekuwa likifanya mashambulio ya kuvizia tangu wakati huo.
Wanamgambo hao wanaaminiwa kufanya mashambulio kadhaa
pia katika nchi jirani ya Somalia kama vile Kenya, Uganda na
Tanzania kama njia ya kulipiza kisasi kwa kuingia majeshi ya
Umoja wa Afrika nchini Somalia.
Sign up here with your email