MKE NA HAWARA WAZICHAPA ....MUME ADAIWA KUINGIZA MCHEPUKO NDANI, MKE AKASHTUKA...TIMBWILI LIKAANZA HAPO



KUNA matukio ambayo kama binadamu 

yasikie kwa wengine tu lakini yasikutokeewewe!
 Kama hili la mkazi wa Ukonga –Mzambarauni, 
Dar, Paulo Ndulu ambapo mkesha wa kuamkia 
Sikukuu ya Sabasaba, alijikuta katika wakati 
mgumu pale alipoingia kibaruani kuamua ngumi
 kati ya mkewe, Anitha Mapunda na Elizabeth 
Chacha aliyedaiwa kuwa ni hawara yake, OFM
 walishuhudia.
Bw. Paulo Ndulu  akijaribu kuamua ugomvi kati
 ya mkewe,
 Anitha Mapunda na Elizabeth Chacha (mwenye shati 
nyekundu) anayedaiwa kuwa ni hawara yake.
OFM ni kikosi cha kifichua maovu cha Global Publishers ambacho 
katika kipindi hiki cha Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan 
kimekuwa kikizunguka usiku ili kuhakikisha hakuna watu 
wanaokwenda kinyume na swaumu za Waislam.
.
..Iilikuwa ni soo la kufa mtu.
OFM MITAANI USIKU
Siku ya tukio, majira ya saa nane usiku, OFM ilikuwa ikikatiza maeno ya Ukonga jijini Dar na kubahatika kushuhudia timbwili zito sana kutoka kwenye nyumba ya Ndulu huku majirani kibao wakiziba mtaa kushuhudia.

Bw. Paulo Ndulu akiendelea kuamua ugomvi huo.
OFM ilisogea kwenye sekeseke hilo na kugundua kuwa, ndani ya
 nyumba ya Ndulu kulikuwa na kasheshe zito la nguo kuchanika
 kati ya wanawakwe wawili ambapo majirani walisema mmoja ni
 mke, mwingine hawara, kisa?
...Mara majirani nao walishuhudia ugomvi uliokuwa
 ukiendelea
 kwa kupiga chabo dirishani.
MSIKIE JIRANI
“Mke aliaga anasafiri, mume akaingiza mwanamke mwingine, 

sasa kumbe mke hakusafiri kikweli, alimdanganya mumewe 
baada ya kujua kuna mwanamke atakuja,” alisema jirani mmoja
 huku akilalamika kwamba, amepika daku linapoa kwa sababu 
ya kushuhudia filamu hiyo ya bure.
Ilidaiwa kuwa, Anitha alikuwa katika wakati mgumu baada ya 

mumewe kuwa na tabia ya kumwingiza mwanamke huyo ndani 
na kumwambia yeye akakae mahali anywe soda au aende kwao 
mpaka mgeni wake atakapoondoka ndipo arudi.
Bw. Paulo Ndulu akizidi kumsihi mkewe apunguze 
munkari.
ALIJIFICHA
Siku ya tukio, kwa mujibu wa mashuhuda, Anitha alipobaini ujio

 wa mgeni huyo (Elizabeth) alijifanya anakwenda Kimanzichana, 
Kisarawe, Pwani lakini uhalisia alikwenda kujificha nyumba ya
 jirani huku akiweka wapambe wampigie chabo nyendo za mumewe
 kwa usiku huo kwa sababu alikuwa amechoshwa na uonevu wa
 kutakiwa kwenda kukaa mahali.
Bi. Anitha Mapunda(mke wa Paul Ndulu) akiwa ni 
mwenye
 ghadhabu kubwa.
MUME ARUDI, HAWARA ATINGA
Chanzo kilisema saa moja usiku, Ndulu alionekana akirudi nyumbani
 hapo. Muda si mrefu, mrembo mweupe, mrefu alionekana akiingia 
nyumbani hapo na Ndulu alitoka kumpokea.
Makamanda wa OFM wakimdhibiti hawara alipotaka
 kukimbia.
WAPAMBE WANYAKUA VIATU VYA ELIZABETH
Jirani huyo alizidi kusema kuwa, wakati Eliza akizama ndani Ndulu

, alivua viatu na kuviacha nje ya mlango. Wapambe wakavichukua na
 kwenda kumuonesha Anitha akiwa mafichoni ili kumthibitishia kuwa
 tayari mumewe alikuwa na kifaa ndani.
...Hawara huyo(Elizabeth Chacha) akikalishwa chini 
ili wayamalize kiutu uzima.
Baada ya kuoneshwa viatu hivyo, Anitha alichanganyikiwa na kutoka
 kwenda nyumbani kwake ambapo aliingia na kusababisha varangati
 hilo la aina yake lililodumu kwa karibu dakika ishirini mpaka OFM 
ilipotokea ambapo pia askari wa kulida doria usiku walitinga eneo la
 tukio.
Bi. Elizabeth chacha akisikiliza kwa hofu uamuzi
 uliochukuliwa.
MJUMBE ASHIRIKISHWA
Ili kuweka sawa mambo ya kisheria, maafande hao wenye maadili

 ya kazi walikwenda hadi kwa Mjumbe wa Shina Namba 29, Mama
 Urio ambaye waliongozana naye mpaka kwenye eneo lenye kizaazaa.
Hata hivyo, polisi na mjume huyo walimkuta Anitha ameshamvaa 
mbaya wake huyo huku akimtupia maneno yenye lawama na shutuma nzitonzito kwamba anamvunjia nyumba yake.
...Majirani walifika eneo la tukio na kushudia mkasa huo.
WATU DIRISHANI WEWEEE!
Ndulu mbali ya kuchoka hoi kufuatia kazi nzito na kumdhibiti mkewe asiendelee kuzichapa na Eliza, pia alikuwa na kazi nyingine ya kugombana na majirani ‘wambeya’ walijaa dirishani kwa nje wakimporomoshea maneno yenye kuudhi.

wananchi akiendelea kujionea laivu yaliyojiri.
UTETEZI WA NDULU
Baada ya hali ya hewa kutulia, polisi walimuhoji Ndulu kuhusu

 sakata hilo, alikiri kuishi na Anitha kwa zaidi ya miaka minne
 lakini alimkana kuwa si mkewe kwa kuwa yeye ni Mkristo wa ma
dhehebu ya Katoliki na hakuwahi kufunga naye ndoa.
Bw. Paulo Ndulu akijaribu kuwafukuza mashuhuda wa tukio hilo la aibu.
Hata hivyo, utetezi huo wa Ndulu ulipingwa vikali na mjumbe wa nyumba kumi na polisi ambapo walimwambia kisheria mwanaume na mwanamke wakiishi ndani ya nyumba kwa muda huo tayari ni mkewe.
Wakasema kwa hiyo kitendo cha kumpelekea mwanamke mwingine ndani ni kutafuta machafuko kwa makusudi.

Bw. Paulo Ndulu akijitetea kuhusu uhusiano wake na hawara huyo.
ELIZABETH SASA
Wakati wote wa sakata, Elizabeth alikuwa akipiga mayowe ya kuomba msaada akisema amekoma kwani Ndulu alimwambia kuwa haishi na mwanamke baada ya kuachana na Anitha muda mrefu kwa sababu za ugumba.

Bi. Elizabeth Chacha akiondoka peku peku eneo la tukio.
"Mimi aliniambia haishi na mwanamke na nilimuuliza sana kuhusu hili naye akanithibitishia kuwa ni msela lakini hata hivyo machale yalikuwa yakinicheza muda wote, namuomba radhi mwanamke mwenzangu jamani,” alisema Eliza.

MWISHO WA SAKATA
Hatima ya sakata hilo, Elizabeth alitakiwa kurudi kwao, Ubungo 

-Maziwa jijini Dar na Anitha alishauriwa kwenda kulala kwa kaka yake anayeishi jirani na eneo hilo chini ya usimamizi wa mjumbe.
ANITHA MWENYEWE
Akizungumza na OFM baada ya kutulia kwa sekeseke, Anitha alisema miaka minne ya maisna na Ndulu, mapenzi yalikuwa motomoto lakini siku za  karibuni mwanaume huyo alibadilika ghafla, akaamini ni baada ya kumpata Eliza.
Previous
Next Post »

Blogger templates