Mtangazaji anayedili zaidi na mambo ya haki za
wanawake
Bongo, Joyce Kiria.
SOO! Mtangazaji anayedili zaidi na mambo ya haki za wanawakeBongo, Joyce Kiria amenagwa na watu mbalimbali mitandaoni
kwa kile kinachoonekana kuingilia sakata la mwimbaji wa Injili
nchini, Flora Mbasha na mumewe Emmanuel Mbasha, akionekana
zaidi kumtetea Flora.
Mmoja wa watoa maoni katika mtandao wake aliandika: “Joyce
acha kujidhalilisha, huoni kama unapoteza utu wako? Naanza
kuamini kuwa na wewe ni miongoni mwa wasioheshimu ndoa zao
kutokana na kuwashauri wenzako upumbavu!
“Kwa mantiki hiyo hustahili hata kuwepo kwenye Kipindi cha
Wanawake Live, ikiwa unatetea upumbavu. Acha kuingilia
mambo yaliyopo mahakamani, utapoteza mashabiki wako bure.”
Licha ya kunangwa kwa maneno makali mara kwa mara, Joyce
ameendelea kuandika kila wakati kuhusiana na ishu hiyo,
akionyesha hisia zake waziwazi kuwa yupo upande wa Flora
jambo ambalo limepingwa vikali na wachangiaji walio wengi,
wakimtaka asijadili suala lililopo mahakamani
Sign up here with your email