MUDA WA NYONGEZA KWA WAOMBAJI MIKOPO AMBAO HAWAKUJAZA FOMU ZA MAOMBI YA MIKOPO KABLA YA JUNI 30, 2014

index
Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu inawafahamisha
 waombaji wa mikopo kwa mara ya kwanza na Umma kwa ujumla 
kwamba muda wa maombi ya mikopo umeongezwa kwa mwezi mmoja
 kutoka Julai 1, 2014 hadi Julai 31, 2014.
Bodi ilianza rasmi kupokea maombi ya mikopo kwa njia ya mtandao
 kuanzia Aprili 23, 2014 ambapo tarehe ya mwisho wa kupokea maombi
 hayo ilikuwa Juni 30, 2014.Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya 
Juu imetoa muda wa nyongeza kwa waombaji wa mikopo kukamilisha 
maombi ya mikopo katika kipindi cha siku 30, kupitia mtandao kwa anuani: http://olas.heslb.go.tz.

Mwombaji wa mkopo atakayekumbana na matatizo ya kiufundi wakati 
wa kujaza fomu yake apige simu kwenye dawati la msaada la Bodi kupitia
 namba 022 550 7910 kuanzia Jumatatu hadi Ijumaa saa 2.00 asubuhi 
hadi saa 2.00 usiku, na Jumamosi kuanzia saa 2.00 asubuhi hadi saa
 10.00 jioni.
Tarehe ya mwisho ya kupokea maombi hayo kwa njia ya mtandao ni 
31 Julai 2014 na hakutakuwa na muda mwingine wa nyongeza baada
 ya tarehe hiyo kupita.
IMETOLEWA NA:
KAIMU MKURUGENZI MTENDAJI
BODI YA MIKOPO YA WANAFUNZI WA ELIMU YA JUU
Previous
Next Post »

Blogger templates