JESHI la Polisi Mkoa wa Arusha linamsaka kwa udi na uvumba,
muuza nyama jijini hapa, Lucas Lomayany Molel (37) mkazi wa
Ilboru kwa madai ya kumuua mkewe wa ndoa, Agnes Lucas (24)
kwa kumcharanga na sime kwa kile kinachoelezwa kuwa ni
kutokana na wivu wa mapenzi.
Dada wa Lucas Lomayany Molel (37) anayesakwa
kwa kumuua mkewe wa ndoa, Agnes Lucas (24), akiwa
katika chumba kilichotumika kwa mauaji hayo.
Chanzo cha habari kimeliambia Amani kuwa, tukio hilo la kutisha
lilitokea usiku wa kuamkia Julai 7, mwaka huu, nyumbani kwa
mtuhumiwa ambapo baada ya kutekeleza mauaji hayo aliufunika
mwili wa marehemu kwa shuka na kuendelea kulala nao kitandani
hadi alfajiri alipotoroka.
Akisimulia kuhusu mauaji hayo, ndugu wa marehemu aitwaye
Akisimulia kuhusu mauaji hayo, ndugu wa marehemu aitwaye
William Lomayany alisema usiku wa tukio, saa 4, mtuhumiwa
alirejea nyumbani kwake na kutomkuta mkewe, akamsubiri hadi
saa 6 usiku, mke akarejea.
Godoro la kitanda alipokuwa analala marehemu,
Agnes likiwa limechafuka kwa damu.
Alisema marehemu baada ya kufunguliwa mlango na kuingia,
alivua nguo zote na kubaki na ‘kufuli’ ambapo alijifunga kanga
na kupanda kitandani kulala. Mtuhumiwa alimfuata chumbani
na kumhoji kuhusu kuchelewa nyumbani hadi muda huo na
ndipo mzozo ulipoanza.
William alizidi kusema kuwa, wawili hao walianza kugombana
William alizidi kusema kuwa, wawili hao walianza kugombana
kwa maneno lakini baada ya muda hali ya utulivu ilirejea, ndipo
asubuhi ilipopatikana taarifa za kuuawa kwa Agnes jambo
lililotafsiriwa kuwa huenda utulivu huo tayari Agnes alishauawa.
Ndoo ikiwa na damu ya Marehemu Agnes
Lucas.
Inadaiwa kuwa, mtoto wa kwanza wa mtuhumiwa, Jessica Lucas (11)
ndiye aliyekuwa wa kwanza kufungua mlango wa chumbani kwa
wazazi wake na kumkuta mama yake amelala na damu chapachapa,
akaenda kutoa taarifa kwa majirani.
Ilidaiwa kuwa, baada ya taarifa hiyo, majirani waliingia ndani ya
Ilidaiwa kuwa, baada ya taarifa hiyo, majirani waliingia ndani ya
chumba hicho na kuukuta mwili wa marehemu ukiwa umelala
kwenye dimbwi la damu huku akiwa mtupu.
Agnes Lucas, enzi za uhai wake, akiwa kwenye
picha ya pamoja na mumewe, Bw. Lucas Lomayany
Molel.
Akizungumza mbele ya askari polisi waliofika kushuhudia tukio hilo,
Jessica alisema baba yake alimwamsha usiku akimtaka atoke kufunga
mlango baada ya kutoka ndani. Akajua baba yake anakwenda kazini
kama ada.
“Nilikwenda kufunga mlango, baba aliondoka bila kusema chochote.
“Nilikwenda kufunga mlango, baba aliondoka bila kusema chochote.
Lakini jana usiku (Julai 6) baba alimpiga sana mama na alinipiga na
mimi wakati namwambia amsamehe,” alisema Jessica.
Majirani wa wanandoa hao, wamelaani mauaji hayo na kusema Lucas
hakupaswa kumuua mkewe badala yake angewashirikisha watu
wengine wakiwemo wazazi wamkanye kama alikuwa akimsaliti.
“Kwa jinsi Lucas alivyokuwa mpole sikutegemea kama angemuua
“Kwa jinsi Lucas alivyokuwa mpole sikutegemea kama angemuua
mkewe kikatili, kama alikuwa akimsaliti angewaeleza wazazi wake
ili wamkanye,” alisema jirani yao ambaye hakupenda jina lake
liandikwe gazetini.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Liberatus Sabas alikiri kutokea
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Liberatus Sabas alikiri kutokea
kwa tukio hilo na kusema kuwa, uchunguzi unaendelea na jeshi lake
linamsaka mtuhumiwa huyo
Sign up here with your email