PICHA 4:MKE WA MTU ACHANJWA NYEMBE KISA FUMANIZI..SOMA ZAIDI

Rehema Juma (21) ambaye ni mke wa mtu
, mkazi wa Mtaa wa Msamvu B, Kata ya Kihonda
 Maghorofani mkoani Morogoro amechanwa na 
nyembe mwilini na baadaye kutembezwa bila nguo 
mtaani mchana kweupe akituhumiwa kufumwa na mume wa mtu.
...Aliyekatwa nyembe.
 Tukio hilo la aina yake  ambalo lilivuta umati mkubwa,
 lilitokea Julai 5, mwaka huu saa 10 jioni katika Mtaa wa
 Msamvu B.
 Mashuhuda wa tukio hilo walipohojiwa na mwandishi 

wetu walidai kuwa kwa muda mrefu, Zaitun Ally (30) ambaye
 pia anaishi kwenye mtaa huo alikuwa akimshutumu Rehema
 akidai anatembea na mumewe, hivyo akaamua kutega mtego
 bila mafanikio.
 “Zaituni baada ya kushindwa kuwanasa leo aliamua kumuita

 Rehema nyumbani kwake na kudai amewafuma na mumewe 
hivyo kumchana nyembe baadaye kumvua nguo na kumtembeza
 bila nguo mtaani hadi nyumbani kwake umbali wa mita 300 
mchana kweupe,” alisema mmoja wa mashuhuda hao 
aliyejitambulisha kwa jina la Ashura Ally.

Rehema Juma akiwa na mama yake.
 Mwandishi wetu alifika nyumbani kwa Rehema
 na kumkuta akiwa amefungwa bendeji sehemu 
za mwili wake na alipoulizwa alifafanua:
“Ni kweli tukio hilo limetokea lakini siwezi kuzunguma

 peke yangu, twende kwa mama mkwe Mtaa wa Ngerengere.”

Mwandishi wetu na Rehema walipofika kwa mkwe
 wa mtuhumiwa, Lilian Julius Sechonge ambaye ni 
mjumbe wa serikali za mtaa wa Ngerengere na 
kutakiwa kuzungumzia tukio hilo alikuwa na haya ya
 kusema:Mtuhumiwa wa tukio hilo.
 “Ni kweli Rehema ni mkwe wangu kwa mwanangu 
aitwaye Godfrey Sechonge anayeishi naye hadi sasa, 
Julai 5, mwaka huu mwanangu huyo alikuja na 
akaniambia mkewe anatembezwa bila nguo.
“Nilifika eneo la tukio na kumkuta mkwe wangu yuko

 uchi huku akivuja damu mwili mzima.
 “Aliniambia amecharangwa viwembe na Zaituni akimshutumu

 kutembea na mumewe, nilimchukua mwanangu na kumkimbiza
 polisi ambapo tulipewa PF3 na kufunguliwa jalada namba
 MOR/RB/4009/2014.”
Naye Rehema alipozungumzia kisa hicho alisema siku ya tukio

 saa 4 asubuhi, Zaituni alimtuma mwanaye nyumbani kwake na
 kumuomba aende kwake (Zaituni).
 “Nilipofika kwake aliniingiza ndani na kuniwekea kisu shingoni

 huku mwanaye akinirekodi na simu yake, akaniuliza nimetembea
 mara ngapi na mumewe!
“Alitaka kujua pia amenihonga shilingi ngapi, kwa hofu ya kuchinjwa

 nilikubali kwamba nilitembea naye mara moja na alinipa shilingi elfu 
tano. “Baada ya kusema hivyo akaniachia, nikarudi nyumbani.

Saa kumi aliniita tena, nilipofika nikamkuta yuko na mumewe na
 watoto wao, akaniuliza unamjua huyu? Nikamwambia simjui, 
akatoa simu na kufungua mahojiano, mumewe alipojaribu kumpora,
 akamchanja na wembe.
Mtuhumiwa akihojiwa.
 “Ghafla akahamia kwangu na kuanza kunichanja kwa wembe
 huku nikipiga kelele na akanivua nguo kisha akanitoa nje na 
kunipeleka kwangu nikiwa na nguo ya ndani tu,” alisema Rehama.            
Akizungumza na mwandishi wetu diwani wa kata hiyo, 

Lydia Mbihaji alisema tangu aanze kuongoza watu hajawahi 
kukutana na tukio kama hilo ambalo aliliita ni la kinyama.
Tayari Rehema amelifikisha sakata hilo polisi na Zaituni alikamatwa

 na kuwekewa dhamana na mumewe akisubiri kuburuzwa mahakamani
 wakati wowote.
 Baada ya kudhaminiwa, mwandishi wetu aliwashuhudia Zaituni

 na mumewe wakizungumza na Rehema ambapo inadaiwa wanataka
 ipatikane suluhu kabla kesi haijaanza kuunguruma mahakamani.
Previous
Next Post »

Blogger templates