Wasichana
zaidi ya 200 wa Chibok waliotekwa na kundi la Boko Haram wanadaiwa kuwa
katika hali mbaya na ya kutisha zaidi. Senator wa jimbo la Borno
anasema hufanyiwa vitendo vya kinyama kupita maelezo.
Akifanya
mahojiano na kituo cha runinga cha Sahara TV, Senator Khalifa Ahmed
Zanna wa Borno Central amesema amepata ripoti mpya kuwa wasichana hao
waliotekwa siku zaidi ya 70 zilizopita hubakwa na wafuasi wa kundi hilo
huku wakichukuliwa video ambayo baadae huoneshwa hadharani.
Senator
huyo ameeleza kuwa ingawa hakushuhudia video hiyo lakini mtu
aliyemsimulia matukio hayo alikuwa na video hiyo na alieleza kuwa
msichana akimaliza kubakwa hupiga magoti mbele ya mbakaji na kumuomba
amhurumie.
“Therefore
the girl after being raped, she curled down to the man, kneeling down
and begging him to please be patient. So disturbing. And although I
didn’t see the video, the person narrated to me, he said he had the
video, and he was narrating to me, and look at the situation.” Amesema Senator Khalifa.
Amesema mbali na wasichana hao waliotekwa, kundi hilo limewakamata wanawake zaidi ya 500 wanaokutwa barabarani au vijijini.
Mbali
na tukio hilo la kinyama, amesema ripoti aliyopewa inaonesha kuwa kundi
hilo hivi sasa halina chakula cha kutosha hivyo linaingia vijijini na
kuwanyang’anya wanakijiji chakula walichonacho huku wakifanya matukio ya
kinyama.
Kufuatia
matukio hayo wanakijiji wengi wamekimbia makazi yao na kuhamia mijini
bila kujua hatima yao huku wengine wakiingia kwenye nchi za jirani.
Sign up here with your email