Mwanamke
mmoja ameripotiwa kumchoma kisu na kumuua mwalimu wa kike wa shule ya
msingi mbele ya wanafunzi wake katika mji wa Albi ulio kusini mwa
Ufaransa.
Muendesha
Mashtaka wa Albi, Claude Derens ameiambia AFP kuwa tukio hilo limetokea
jana (July 4) majira ya asubuhi kwa saa za Ufaransa na kwamba uchunguzi
unafanyika ili kubaini sababu zilizopelekea mwanamke huyo kufanya tukio
hilo la kikatili.
“Mama
huyo alionekana akiwa na kisu na akamchoma mwalimu wa kike mwenye umri
wa miaka 34 mbele ya wanafunzi wake, sababu itafahamika baada ya
uchunguzi kukamilika.” Claude Derens aliiambia AFP.
Aliongeza
kuwa baada ya tukio hilo, rais wa Ufaransa Francois Hollande alimtuma
waziri wa elimu, Benoit Hamon haraka katika shule hiyo ili kuhakikisha
anachukua hatua kama mwakilishi wa serikali.
Sign up here with your email