Sakata la Flora Mbasha na Mumewe lamtokea puani Joyce Kiria

Mtangazaji anayejihusisha zaidi na mambo ya haki za wanawake Bongo, Joyce Kiria amenangwa na watu mbalimbali mitandaoni kwa kile kinachoonekana kuingilia sakata la mwimbaji wa Injili nchini, Flora Mbasha na mumewe Emmanuel Mbasha, akionekana zaidi kumtetea Flora.
 
Mmoja wa watoa maoni katika mtandao wake aliandika: “Joyce acha kujidhalilisha, huoni kama unapoteza utu wako? Naanza kuamini kuwa na wewe ni miongoni mwa wasioheshimu ndoa zao kutokana na kuwashauri wenzako upumbavu!
 
“Kwa mantiki hiyo hustahili hata kuwepo kwenye Kipindi cha Wanawake Live, ikiwa unatetea upumbavu. Acha kuingilia mambo yaliyopo mahakamani, utapoteza mashabiki wako bure.”
KIRIA
Licha ya kunangwa kwa maneno makali mara kwa mara, Joyce ameendelea kuandika kila wakati kuhusiana na ishu hiyo, akionyesha hisia zake waziwazi kuwa yupo upande wa Flora jambo ambalo limepingwa vikali na wachangiaji walio wengi, wakimtaka asijadili suala lililopo mahakamani.
Previous
Next Post »

Blogger templates