Mji wa Dodoma unakua kwa kasi kubwa, ofisi za serikali na taasisi zisizo za kiserikali zinajengwa kwa wingi.
Wafanyabiashara
nao hawapo nyuma wakiwamo wanaonadi miili yao kama bidhaa. Hawa ni
maarufu kwa majina kama vile makahaba, machangudoa na dada poa.
Kimsingi,
wauza miili wanavutiwa na mengi mjini Dodoma, ikiwamo ongezeko la watu
linalosababishwa na kuwepo kwa taasisi za elimu ya juu.
Pia
shughuli nyingi za kijamii na kitaifa zimekuwa zikifanyika mjini hapo,
hivyo kuvutia watu wengi wakiwamo wafanyabiashara hawa.
Kushamiri kwa biashara ya ukahaba kumewafanya wahusika kutafuta ‘sumaku’ ya kuvutia wateja.
Uchunguzi
wa Mwananchi umebaini mojawapo ya njia wanazotumia kupata wateja ni
kujinadi kuwa wao ni wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma (Udom).
Ni
kwa sababu hii, chuo hicho ambacho kimsingi kimebadili maisha ya
kijamii na kiuchumi ya mji wa Dodoma, mara kwa mara kimekuwa kikikumbwa
na kashfa ya wanafunzi wake kujihusisha na vitendo vya ukahaba.
Udom na ukahaba
Baadhi ya watu waliohojiwa wanasema makahaba wengi wanatumia jina la chuo hicho kama ‘ndoano’ ya kuwanasa wanaume.
Na
kwa hakika mkakati wao huu unaonyesha kufanikiwa, japo kwa upande
mwingine umekuwa na matokeo hasi kwa jamii ya chuo hicho kinachoongoza
kwa kuwa na wanafunzi wengi nchini.
Moja
ya maeneo ya starehe ambayo makahaba hawa wamegeuza kuwa vijiwe vyao
vya kawaida ni pamoja na klabu moja ya starehe maarufu iliyopo eneo la
Makole.
Baadhi
ya wateja waliohojiwa klabuni hapo wanasema hawana uhakika wa
wanafunzi kujihusisha na biashara hiyo, na kuwa maneno ya wanafunzi wa
Udom kuhusishwa na ukahaba yamekuwa katika midomo ya wakazi wengi mjini
hapo, lakini bila ya kuwa na ushahidi.
Mmoja
wa wateja ambaye hakupenda kujitambulisha jina lake, alisema upo
uwezekano wa makahaba kutumia jina la chuo kwa minajili ya kushawishi
mteja na kuficha utambulisho halisi.
“Kahaba
anajisikia ujiko (sifa) sana kujitambulisha kuwa ni mwanafunzi wa Udom
kutokana na sifa ya chuo hicho kuwa na wasichana wazuri sana,” anasema.
Kwakweli
hata mimi binafsi nishawasikiaga mademu kibao ukikutana nao sehemu
ukimuuliza tu we nani na wafanya nini now utaskia tu ooh nasoma Udom
then ukimuuliza mbona uko apa Dar na vyuo bado havijafungwa ataanza
kujiumauma tu lol haa ahaaa TUMEWASTUKIAAA..
Sign up here with your email