MADAI YA KUCHEPUKA KAJALA ACHARUKA

Kajala Masanja akiwa kwenye pozi

BAADA ya kuzagaa kwa taarifa mbalimbali kwamba mwigizaji wa Bongo, Kajala Masanja anachepuka nje, ameibuka na kukanusha madai hayo akisema hayana ukweli wowote. 
Mwigizaji wa Bongo movie Kajala Masanja
Mitandao mbalimbali ya kijamii imekuwa ikiposti taarifa mbalimbali zinazomhusisha Kajala kutembea na wanaume tofauti kitu ambacho mwenyewe amesema hakina ukweli na wanaosambaza uvumi huo, wakome.
Akizungumza na mwanahabari wetu Julai 3, mwaka huu alisema wanaoeneza habari za yeye anachepuka wanamtafuta ubaya kwani hana mpango wowote wa kuolewa wala kuishi na mwanaume kwa sasa.
“Waniache, mtu akisema nina mwanaume alishawahi kuniona? Sina mwanaume mwingine zaidi ya mume wangu,” alisema Kajala.
Kwenye mahojiano hayo, Kajala alisisitiza kuwa, haoni sababu ya yeye kuchepuka wakati mumewe Faraja Augustino yupo hai na anaamini ipo siku atatoka gerezani na ataendelea na maisha ya ndoa yake kama ilivyokuwa zamani.
“Kiukweli sioni haja ya kuolewa na mwanaume mwingine tena wakati ni wazi ipo siku mume wangu atakuwa huru, naomba ieleweke kwamba sina mpango na mwanaume yeyote na sasa namgonjea atoke tuendelee na maisha yetu,” alisema Kajala.
Mume wa Kajala, Faraja Agustino anatumikia kifungo cha miaka 7 baada ya kushindwa kulipa faini ya shilingi milioni 200 kufuatia kesi ya kutakatisha fedha iliyokuwa ikimkabili.
Kwenye kesi hiyo, Kajala ambaye naye alihusishwa, alilipiwa faini ya shilingi milioni 13 na mwigizaji Wema Sepetu, kifungo cha miaka mitano kikamuepuka.
Previous
Next Post »

Blogger templates