SOMO KWA WENGINE:MTOTO WA RAIS ANASWA AKIPIMA NGOMA

Mwandishi wetu alimshuhudia Amini akiwa
 katika kituo hicho kupima ugonjwa huo katika
 siku hiyo ambayo huadhimishwa kama Siku ya 
Wapendanao ‘Valentine’s Day’ ili kutaka kujua
 afya yake na kuwa tayari majibu yake yawekwe hadharani.
Hata hivyo, baada ya vipimo na kutakiwa 
kusubiri majibu, Amini alionekana kuwa 
mnyonge na mwenye mawazo mengi ingawaje
 aliweza kujifariji kwa kuangalia runinga iliyopo
 katika chumba cha kusubiria majibu.
Alipoitwa kwenda kupatiwa majibu yake
 alijikuta akijikwaa zaidi ya mara tatu na
 alipoingia chumba cha majibu, nusura 
adondoke baada ya kujikwaa tena katika
 kizingiti cha mlango wa kuingia kwa daktari.
Mara baada ya kupewa majibu yake,
 Amin alisema amechukua uamuzi 
wa kuijua afya yake siku hiyo kwa 
sababu vijana wengi huitumia kwa
 ajili ya kufanya ngono katika nyumba za kulala wageni.
“Nimeamua kupima Ukimwi leo kwa sababu
 vijana wengi wamepanga kukutana na 
mpenzi wao kwa lengo la kufanya ngono,”
 alisema Amini ambaye alionekana kuwa 
na furaha baada ya kupata majibu mazuri.
Previous
Next Post »

Blogger templates