Baadhi ya madenti wa vyuo vikuu mbalimbali jijini Dar es Salaam, wameoza kwa matukio machafu ya ngono.
Katika
uchunguzi wa muda mrefu, Inaonyesha kuwa kuna kamtindo ka wanafunzi
kufanya mapenzi ndani ya hostel zao huku wakijirekodi na kupiga picha
chafu na za aibu na wengine hata kuuza miili yao ili kukidhi hali ngumu
ya maisha iliyopo vyuoni
Data
zilizokamilika zilionesha kuwa wanafunzi hao waliojulikana kwa jina
mojamoja ni Maya mwenye umri wa miaka 19, anayesoma katika chuo maarufu
cha mahesabu, Raya anayebukua masomo ya Information Technology (IT) na
mwingine ambaye jina lake na chuo anachosoma havikupatikana. Habari
zilidai kuwa Raya na rafiki zake watatu wamekuwa wakijihusisha na
vitendo haramu vya ngono rejareja na mwanaume mmoja wakiwa katika
hosteli hiyo kwa kigezo cha mshiko ‘mnene’ wanaochuma kwa jamaa huyo. Hata
hivyo, ripoti ya uchunguzi wetu haikufanikiwa kuwanasa wakimhudumia
mwanaume huyo kwa mpigo, isipokuwa ilifuma picha ambazo kila mmoja yuko
na jamaa huyo kwa nyakati tofauti.Baada
ya kunasa picha hizo chafu kupita maelezo kwa jamii ya Kitanzania,
wapekuzi wetu waliwatafuta wahusika ambapo walifanikiwa kumpata Raya
ambaye pamoja na kuelezwa kuwa kuna ushahidi wa picha, alikana
kuzifahamu. Mbali na matukio
hayo yaliyosheheni katika makabrasha yetu, uchunguzi ulibaini kuwa, siyo
kila mwanachuo anayepata nafasi hiyo adimu ya kujiunga na elimu ya juu
anafanya kile kilichokusudiwa, badala yake wanafanya kinyume kwa
kujihusisha na vitendo haramu na hatarishi vya ngono.
Imebainika
kuwa wanaoishi hosteli ndiyo wanaoongoza kwa uchafu huo kwa sababu wana
uhuru wa kufanya hivyo bila kubanwa hivyo kugeuza vyumba vyao
madanguro.
Katika
uchunguzi wetu, ilibainika pia kuwa idadi kubwa ya wasichana wanaojiuza
katika viunga mbalimbali jijini Dar ni wanafunzi wa vyuo vikuu
wanaofanya biashara haramu ya kuuza miili kwa wanaume ili kukidhi
mahitaji ya kila siku kuendana na mfumuko wa bei.
Wakijitetea
kwa sharti la kutotajwa , madenti wa vyuo walionaswa wakijiuza katika
eneo la Sinza Afrika Sana, Dar hivi karibuni, walidai tatizo ni Bodi ya
Mikopo ya Elimu ya Juu ambayo haiwapi fedha za kutosha
Sign up here with your email