Wakati anazungumzia kilichomsababisha ajiingize kwenye kazi hiyo alisema ni ugumu tu wa maisha ndio sababu kubwa.
Alisema
hakuweza tena kuwahudumia watoto wake wanne ambao walikuwa wametelekezwa
na baba yao mzazi, kulipa kodi ya nyumba nayo ulikuwa mtihani.
Akizungumzia
jinsi alivyokutana na jamaa aliyemshawishi kufanya biashara hiyo
alisema kuwa, aliahidiwa kusaidiwa kutatua matatizo aliyonayo na kweli
jamaa alifanya hivyo huku akimhahidi kumpa biashara ya kusafiri.
Baadae
alipokuja kujua ni biashara ya kusafirisha madawa, dada huyo alikataa
kuifanya lakini alipata vitisho vikali toka kwa jamaa aliyemgharamia na
kumtaka arudishe gharama zake.
Hakuwa na
jinsi, hakuwa hata na senti tano nyeusi ya kulipa, basi ikambidi afanye
biashara ndipo ikambidi ashindie gramu 685 za unga ukeni.
Ni
mwanamke wa kinaijeria Chinelo Okorom, 36, muuza chakula mitaani
aliyekamatwa katika uwanja wa ndege wa Murtala Muhammed International
Airport huko Ethiopia alipokuwa akisafirisha unga toka Nigeria kuingiza
Ethiopia, unga aliokuwa ameushindia ukeni. Brimtime
Sign up here with your email