MBALI na
Askofu wa Kanisa la Full Gosple Bible Fellowship, Zacharia Kakobe
kuteswa na misukule inayodaiwa kufufuliwa na baadhi ya makanisa ya
kiroho nchini, Mchungaji wa Kanisa la Maombezi, Anthony Lusekelo ‘Mzee
wa Upako’ (pichani) naye ameibuka na kucharukia suala hilohilo.
Akizungumza
na Uwazi juzi, Mzee wa Upako alisema suala la misukule linamtesa sana na
kwamba anapingana na kufufuliwa kwao na baadhi ya wachungaji wa
makanisa mbalimbali wanaojigamba kufufua misukule wakati si kweli na ni
utapeli mtupu.
MZEE WA UPAKO ANAFUNGUKA:
“Kuna baadhi ya viongozi wa makanisa ya kioroho (bila kutaja majina) wanadanganya watu kuwa wanatoa misukule, si ukweli kabisa ni uongo. Wanatafuta namna ya kula sadaka za waumini wao kwa kuonekana wanaweza sana mambo ya kiroho,” alisema Mzee wa Upako na kuongeza:

“Hawa
wachungaji wanatuchafua sana sisi tunaosimamia Neno la Mungu, wanaharibu
Kanisa la Mungu kwa kudanganya waumini wao kwa sababu ya pesa tu. Hebu
fikiria kuna wengine wanatoa hadi shilingi 400,000 kwa mtu ili akubali
kufanywa msukule feki na baadaye aombewe kanisani tena nimesikia
wanatengenezewa hati za kifo kuonesha kuwa kweli watu hao walifariki
dunia wakati si kweli, wamwogope Mungu.
“Huo ni
usanii ndani ya Kanisa la Mungu. Nasema naumizwa sana na wachungaji wa
namna hii, nateseka sana na hili jambo. Ninayo mpaka CD za mahubiri za
baadhi ya viongozi wa makanisa wanaodanganya kuwafufua misukule lakini
kwa busara siwezi kuwataja ila wanajijua kwa sababu hata dhamira zao
zinawashuhudia.”
TURUDI KWA KAKOBE
Akikazia zaidi, Askofu Kakobe alisema, anayedai ana uwezo wa kufufua misukule ni muongo na kwamba atakuwa anaabudu shetani.
“Mwenye
uwezo wa kufufua ni Yesu Kristo pekee na alifanya hivyo kwa sababu ya
utukufu wa Mungu na si vinginevyo, si binadamu wa kawaida ambaye
amepewa upako wa Mungu anadanganya watu kuwa anao uwezo wa kumtoa mtu
ambaye alichukuliwa msukule,” alisema Askofu Kakobe huku akisisitiza
kwamba mtumishi yeyote wa Mungu anaweza kufanya muujiza huo kwa utukufu
wa Mungu lakini si kwa sababu ya kuonesha yeye anaweza
Akikazia zaidi, Askofu Kakobe alisema, anayedai ana uwezo wa kufufua misukule ni muongo na kwamba atakuwa anaabudu shetani.
Sign up here with your email