BODI YA MIKOPO YA ELIMU YA JUU (HESLB) YATOA KAULI KUHUSIANA NA KUCHELESHWA KWA POSHO YA MAFUNZO KWA VITENDO


Bodi ya mkopo ya Elimu ya Juu nchini Tanzania (HESLB) inashughulikia tatizo la wanafunzi wanaokwenda kwenye mafunzo kwa njia ya vitendo ikiwa na baada ya kulalamikiwa na jumuiya ya wanafunzi wa Elimu ya Juu nchini (TAHLISO).


Akizungumza na East Africa Radio , Mkurungenzi Msaidizi wa Habari, Elimu na Mawasiliano wa Bodi hiyo, Bw. Cosmas Mwaisobwa amesema wanatambua kuchelewa kwa fedha hizo kwa baadhi ya wanafunzi katika programu tofauti katika vyuo vikuu nchini ambapo jitihada zinafanywa na Bodi hiyo kutatua tatizo hilo kwa ili wanafunzi waweze kuendelea na mafunzo yao kwa vitendo.

Hata hivyo Bw. Mwaisobwa hakutoa muda kamili ambao tatizo hilo litashughulikiwa na wanafunzi hao kupatiwa fedha kwa ajili ya mafunzo kwa njia ya vitendo
Previous
Next Post »

Blogger templates