Mabingwa: Chelsea wakishangilia kombe la vijana chini ya miaka 21 kutoka timu za ligi kuu msimu wa 2013/14
MSIMU huu uongozi wa ligi kuu unatarajia kuzindua mashindano mapya ya kombe la ulaya kwa timu za ligi kuu nchini England chini ya miaka 21 na timu kutoka nje ya England.
Vikosi vya vijana chini ya miaka 21 kutoka timu nane (8) za juu katika msimamo wa ligi kuu Engalnd zikiwemo klabu za Manchester City, Manchester United na Chelsea vitashiriki pamoja na timu nane (8) kutoka nje ya England ambapo jumla ya timu itakuwa ni 16.
Hii hatua ni kutekeleza mkakati maalumu wa soka la vijana ulioanzishwa mwaka 2011 ili kuwaimarisha vijana wanaozalishwa na klabu za juu za England.
TIMU 16 ZITAKAZOSHIRIKI
Liverpool, walioshiriki ligi ya vijana chini ya miaka 21 msimu uliopita hawatashiriki mashindano hayo na badala yake nafasi hiyo imeenda kwa West Ham waliomaliza nafasi ya tisa katika msimamo msimu uliopita.
Mashindano hayo yataenda sambamba na ligi ya vijana chini ya miaka 21.
Kwa sasa yatawavutia watu wengi zaidi kwasababu Sky Sports na BT Sports watarusha ‘Laivu’ mechi 10.
Waandaaji wana matumaini kuwa michuano hii itawavutia watu wengi na timu zitapata wachezaji wao wazuri ili kuwaingia katika timu za wakubwa.
Mkurugenzi wa akademi ya Schalke ,Oliver Ruhnert alisaidia kuzalisha wachezaji wanne walioisadia Ujerumani kutwaa kombe la dunia mwaka huu na timu yake itashiriki michuano hiyo ya vijana chini ya miaka 21
Sign up here with your email