TFF YAANIKA HADHARANI: YANGA SC WANA HAKI YA KUTOSHIRIKI KAGAME KAMA HAWAJAJIANDAA, HAKUNA KANUNI INAYOWABANA


Boniface-Wambura

Afisa habari na mawasiliano wa TFF, Boniface Wambura Mgoyo
Na Baraka Mpenja, Dar es salaam
BAADA ya Yanga sc kuenguliwa kushiriki michuano ya klabu bingwa kwa ukanda wa Afrika mashariki na kati , maarufu kama Kombe la Kagame, kwa kugoma kupelekea kikosi cha kwanza kama walivyoagizwa, Shirikisho la soka Tanzania TFF, limesema klabu hiyo ina haki kutoshiriki mashindano kama inaona haijajiandaa.
Afisa habari na mawasiliano wa TFF, Boniface Wambura Mgoyo amezugumza na Mtandao huu mchana huu na kueleza kuwa klabu inapokuwa bingwa, hakuna kanuni inayoibana kwamba lazima ishiriki mashindo fulani, bali kama wanaona hawapo tayari wanaweza kuwasiliana na TFF, halafu klabu nyingine inatafutwa.
“Tunachosema ni kwamba klabu inapokuwa bingwa sio kwamba kuna kanuni zinailazimisha kucheza mashindano. Kwahiyo ikiona kwamba haijajipanga kwa mashindano, bado ina haki ya kutuandikia sisi kuwa hawapo tayari kushiriki mashindano na tunatafuta timu nyingine inayokwenda kwenye mashindano,” alifafanua Wambura.
Hata hivyo, Shirikisho la soka Tanzania limeichagua Azam fc kwenda kushiriki mashindano hayo na tayari limeshawaandikia barua baada ya mawasiliano ya pande zote kwenda barabara.
“Ni kweli , CECAFA waliwapa Yanga muda wa kuthibitisha kikosi chao, lakini muda umekwisha, maana yake sasa CECAFA wamefanya uamuzi wa kuwatoa katika michuano ya Kagame kwa uamuzi wa kupeleka kikosi cha pili au mchanganyiko kinyume na kanuni za mashindano. Na hii ililenga kupunguza hadhi ya mashindano,” alisema Wambura.
andrew coutinho
“Kwahiyo CECAFA wakaiondoa Yanga na badala yake sisi tukawaomba watupe hiyo nafasi kwa kutafuta timu nyingine ambayo itatuwakilisha kwa maana ya Tanzania bara, tukasema lazima tuwe na uwakilishi kwenye mashindano hayo na tumewapa nafasi Azam.”
“Tumeshawaandikia barua baada ya kuzungumza nao na ndio watatuwakilisha kwenye mashindano yanayotarajia kuanza Agosti 8
“Cha msingi cha kuelewa ni kwamba kila mashindano yana kanuni zake na taratibu zake. Kila mashindano lazima uwe na sifa ya kushiriki, ukishakuwa na sifa, unatakiwa kufuata kanuni kama zinavyoelezeka”
Aidha, Wambura alisema TFF hawahusiki kwa lolote kuhusu maamuzi hayo kwasababu wao sio sehemu ya waandaaji wa mashindano.
“Sisi kama TFF hatupo kwenye hayo mashindano na waliohusika kuwatoa Yanga ni waandaji wa mashindano, kwahiyo sisi hatuna lingine la kufanya isipokuwa kuwakumbusha watu kuwa wanapokwenda kucheza mashindano wazingatie kanuni na wasitunge kanuni zao, wanatakiwa kufuata kanuni za waandaaji”
Previous
Next Post »

Blogger templates